Timu
ya Tanzania ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 15 iliyoshika nafasi
ya pili katika Michezo ya Afrika kwa Vijana (AYG) iliyofanyika
Gaborone, Botswana inawasili leo (Juni 2 mwaka huu) jijini Dar es
Salaam.
U15
ambayo imeshinda mechi tatu, sare moja na kufungwa moja inawasili
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 12.30 jioni
kwa ndege ya Kenya Airways ikitokea Gaborone kupitia Nairobi.
Tanzania
ambayo imepata medali za fedha kwa kushika nafasi hiyo ikiwa chini
yaKocha Abel Mtweve ilizifunga Afrika Kusini 2-0, Botswana 2-0,
Swaziland 3-0 na ikatoka sare ya bao 1-1 na Mali. Ilifungwa mabao 2-0 na
Nigeria ambao ndiyo walioibuka mabingwa.
Wachezaji
16 waliounda kikosi cha Tanzania ni Adam Shayo, Amani Ally, Amos
Manguli, Amri Nyuki, Amede Amani, Baraka Rashid, David Uromi, Goodlove
Mdumule, Hance Msonga, Kelvin Kamalamo, Makalius Amrin, Nasson Chanuka,
Paulo Ngowi, Petro Shaban, Rajab Mohamed na Thomas Chindeka.
SUFIANI MAFOTO