Na Mwene Said
MSANII
Emmanuel Mbasha (32) ni mume wa Mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha (pichani wakiwa, amefikishwa
katika Maha kwenye shughuli zao siku za nyuma) kama ya Mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na mashitaka mawili
ikiwemo ya ubakaji.
Mshtakiwa huyo ambaye ni mfanyabiashara na mwimbaji alisomewa
mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Wilberforce Luago.
Wakili
wa Serikali Nassoro Katuga alidai kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo mawili
maeneo ya Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam.
Katuga
alidai katika shitaka la kwanza kuwa, Mei 23, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga,
Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria huku
akijua ni kosa alimuingilia kwa nguvu msichana anayedaiwa kuwa shemeji yake
(jina limehifadhiwa).
Katika
shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Mei 25, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, jijini
Dar es Salaam, kinyume cha sheria, mshtakiwa aliumuingilia kwa
nguvu mfanyakazi wake (jina limehifadhiwa).
Hata
hivyo, mshtakiwa alikana mashitaka hayo .
Upande
wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi la dhamana.
Hakimu
Luago alitaja masharti ya dhamana kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili, mmoja
awe mtumishi wa serikali na mwingine kutoka taasisi inayotambulika watakaosaini
hati ya dhamana ya Sh. milioni 5.
Mshtakiwa
alishindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo alipelekwa rumande na kesi iliahirishwa
hadi Juni 19, mwaka huu itakapotajwa.
Mbasha
akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi alisindikizwa katika basi la Jeshi
la Magereza kwa ajili ya kwenda kuanza maisha mapya mahabusu ya Keko, jijini
Dar es Salaam.
CHANZO: BOFYA HAPA