Mwenyekiti
wa Kamati namba sita wa Bunge Maalum la Katiba Stephen Wassira
akiwasilisha maoni ya Kamati yake leo mjini Dodoma kwenye kikao cha
ishirini na mbili cha Bunge hilo.
|
******
Na Magreth Kinabo, Dodoma
WAZIRI
wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Utaribu, Stephen Wassira amesema
Serikali itawasilisha Hati ya Makubaliano ya Muungano katika Bunge
Maalumu la Katiba baada ya siku mbili zijazo.
Wassira
ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati Namba Sita ya Bunge hilo ambazo
zilikuwa zikijadili Sura ya Kwanza na ya Sita za Rasimu ya Katiba,
alitoa kauli hiyo leo baada ya kuzuka mjadala juu ya uwepo wa hati hiyo
na kama ipo kwa nini haijawasilishwa kwa wajumbe wa Bunge hilo.
Mwenyekiti
huyo alitoa kauli hiyo, kabla ya kuanza kutoa taarifa za wajumbe walio
wengi na wachache juu ya majadiliano ya sura hizo.
“Nataka
kuwahakikishia Hati ya Muungano ipo tena ipo katika hali nzuri. Nataka
kuhaidi kwamba hati hiyo itafikishwa katika Dola ya Jamhuri ya Muungano
siku mbili zijazo,” alisema Wassira.
a ya Kwanza na ya Sita za Rasimu ya Katiba,utaendelea hata kama bado hati hiyo haijawasilishwa.
Sitta
alitoa kauli hiyo baada ya mjumbe mmoja wa Bunge hilo, John Mnyika
kuomba mwongozo wa kutaka Bunge hilo, lisiendelee na mjadala wa sura
hizo hadi hati hiyo iwasilishwe Bungeni hapo.
“Mwenye
mamlaka ya kutaka mjadala uendelee ni Kamati ya Uongozi ya Bunge
Maalum la Katiba, hilo, analolisema Mnyika haliwezekani. Tunaliendesha
Bunge hili kwa gharama. Ombi hili litazuiliwa. Hati ya
Makubaliano itawasilishwa kwa wakati wake,” alisema Sitta huku
akisisitiza kuwa hati hiyo haiwazii kuendelea na kazi ya mjadala huo,
hata Kanuni za Bunge hilo hazisemi hivyo.
lAkiwasilisha
maoni ya walio wengi katika kamati yake, Wassira alisema wanapendekeza
neno Shirikisho liondolewe kwa sababu Hati ya Makubaliano ya Muungano
ya mwaka 1964 ndio msingi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
”Hati
ya Muungano ni sheria ambayo haikuanzisha shirikisho kama wajumbe walio
wachache wanavyodai na badala yake ilikusudia kuanzisha Muungano.
Hivyo, kutumia neno Shirikisho ni kwenda kinyume na Makubaliano yaliyopo
katika Hati ya Muungano,” alisema Wassira.
Wassira aliongeza
kuwa mapendekezo ya kuanzisha serikali ya shirikisho yanakinzana na
masharti yaliyowekwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katika Sura 83 kifungu
cha 9(2) kinachokazia uwepo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
”Ingawa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba inadai yalikuwa mawazo ya wananchi; swali
ni kwamba kama wananchi walitoa maoni wangetaka kuvunja Muungano. Je
Tume ingesemaje?. Shirikisho la serikali tatu litasababisha uendeshaji
wa shughuli za umma kuwa na gharama kubwa na hivyo kuwa mzigo wa
kiuchumi kwa wananchi,” alisema.
Alisema,
kwa mfano gharama za sasa za kuendesha taasisi za muungano ni takriban
sh. Trilioni 10.7 kwa mujinbu wa makusanyo ya mapato yote ya ndani ni
sh. Trilioni 12.6 kwa mujibu wa takwimu za bajeti ya mwaka wa
fedha 2011/2012.
“Kuundwa kwa serikali ya muungano kutaongeza gharama na kupanua nakisi ya bajeti,” alisema.
Mwenyekiti
huyo aliongeza kuwa wajumbe walio wengi wa kamati hiyo, wameshangazwa
na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, kudai kwamba muundo wa serikali tatu ni
maoni ya wananchi walio wengi, wakati hakuna ushahidi wa takwimu.
“Mfumo
wa serikali tatu pamoja na kupigiwa debe na Tume ya Mabadiliko ya
Katiba na UKAWA, lakini hakuna ushahidi wa takwimu kuonyesha kuwa
unakubalika kwa wananchi walio wengi. Aidha, kwamba unakubalika na pande
zote za Muungano,” alisema.
Wassira
alisema kwa mujibu wa takwimu za Tume, Zanzibar asilimia 61 inasemekana
walitaka Muungano wa Mkataba; asilimia 31 walitaka muundo wa serikali
mbili.
“Katika
hali hiyo kusema serikali tatu ni mawazo ya wananchi walio wengi wa
wapi? Kwa Tanzania Bara kati ya watu 16,000 waliochangia Muungano, 8,682
ni kutoka Mkoa wa Kigoma pekee na waliosalia ni kutoka mikoa mikoa
mingine iliyobaki.”
“Sasa
kwa takwimu hizi unawezaje kusema watu wengi wanataka serikali tatu?
Suala la msingi hapa ni kwamba mfumo wa kukusanya maoni uliotumiwa na
Tume bila ya kujali ukubwa au udogo wa sampuli, hauna mamlaka ya
kubadili mfumo kutoka Muungano kuwa Shirikisho,” alisema Wassira.
Aliongeza:
“Hii ni kweli, kwa vile mwaka 1964 Rais Julius Nyerere aliwawakilisha
Watanganyika na Rais Abeid Amani Karume aliwawakilisha Wazanzibar wote
katika makubaliano ya kuunganisha nchi zetu mbili.”
Wassira
alisema kubadilisha hati ya muungano unahitaji kwanza kurudisha Jamhuri
ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, kisha kupitia kura ya
maoni, uamuzi wa mfumo gani wa Muungano na kama ni shirikisho, basi
viongozi wa Tanganyika na Zanzibar wajadiliane aina ya ushirikiano.
Katika
Kamati hiyo, Wassira aliwasilisha maoni ya wajumbe
wachache,ambao walipendekeza Muungano wa Tanganyik na Zanzibar uwe wa
Shirikisho.
Wakati huohuo, Mwenyekiti wa Kamati Namba Saba ya Bunge hilo,kuhusu Sura ya Kwanza nay a Sita, ya Rasimu ya Katiba ,Brigedia Jenerali Mstaafu Hassan Ngiwilizi aliwasisha
maoni ya kamati yake,ambayo pia wajumbe wengi walipendekeza muundo wa
Serikali Mbili na maoni ya wajumbe wachache walipendekeza Muundo wa
Shirikisho lenye Serikali Tatu.