SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, March 17, 2014

Watoto walionyanyaswa na kutelekezwa waanza kupatiwa matibabu

 
John Msumba(03)ameanza kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina na Madaktari baada ya kupigwa kisha kunyimwa chakula na shangazi yake aliyefahamika kwa jina la Mwanahawa Nassoro(32)mkazi wa Airport Kata ya Iyela.

Bibi Lahel Mbembela akilia kwa uchungu mara tu baada ya kumwona mtoto John
Bibi Lahel Mbembela akimkabidhi Muuguzi kiasi cha shilingi 10,000/ kwa ajili ya kumsaidia mtoto huyo
Afisa Ustawi wa Jamii Subira Moses ambaye alisikitishwa na kitendo kilichofanywa na Mwanahawa hivyo aliandika barua ya msamaha wa matibabu ili atibiwe bure ambapo alilazwa Machi 13 Jioni baada ya Madaktari kufanya uchunguzi wa kina.
Joseph Mwaisango akimjulia hali mtoto John kulia ni Msamaria mwema Grolia  Kaguo ndiye aliyejitolea kumhudumia mtoto John
SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kumshikilia Mwanamke mmoja, Mwanahawa Nasoro(32) Mkazi wa Airport Mkoani hapa akituhumiwa  kumtesa na kumnyanyasa mtoto wa kaka yake, Hatimaye mtoto huyo aanza kupatiwa matibabu.

Mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la John Msumba(03)ameanza kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina na Madaktari baada ya kupigwa kisha kunyimwa chakula na shangazi yake aliyefahamika kwa jina la Mwanahawa Nassoro(32)mkazi wa Airport Kata ya Iyela.

Baada ya mtuhumiwa kukamatwa Mtendaji wa mtaa Henry Chaula aliomba msaada kwa wasamaria wema kumkimbiza Hospitali mtoto ili kuokoa maisha kutokana na kuzorota kwa afya kulikotokana na kipigo na ukosefu wa lishe.

Katika Hospitali ya Rufaa alipokelewa na Afisa Ustawi wa Jamii Subira Moses ambaye alisikitishwa na kitendo kilichofanywa na Mwanahawa hivyo aliandika barua ya msamaha wa matibabu ili atibiwe bure ambapo alilazwa Machi 13 Jioni baada ya Madaktari kufanya uchunguzi wa kina.

Hata hivyo Msamaria Mwema Groria Kaguo alijitolea  kulazwa pamoja na  mtoto huyo kwa lengo la kusimamia huduma huku Madaktari na wauguzi wakifanya jitihada kubwa kuokoa maisha ya mtoto huyo kutokana na sehemu kubwa ya mwili wake umeathirika na majeraha yaliyotokana na viboko.

Baadhi ya wasamaria wema Kikiwemo kituo cha Radio cha Bomba FM Mbeya, Gazeti la Jamboleo Mbeya na Mtandao wa Mbeya Yetu wameanza kugharamia fedha za matibabu hayo ambapo dawa alizoandikiwa hazipatikani  Hospitali ya Rufaa na kulazimu kununua kwenye duka nje ya Hospitali.
Mtoto  Baraka Joseph(02) akiwa amelazwa katika hospitali ya Rufaa mbeya
 

Mtoto huyo ambaye aliokotwa na mama lishe anayefahamika kwa jina la Subira Joseph Mwaijulu (Mama Sunche) mkazi wa Nonde Jijini Mbeya,ambaye amekuwa akimhudumia tangu alipotelekezwa amesema kuwa baada ya mtoto kuanza kusumbuliwa na ugonjwa huo aliamua kumpeleka Hospitali ya Rufaa kwa ajili ya matibabu.


Wakati huo huo,Mtoto mwenye umri wa miaka miwili jinsi ya kiume ambaye alitelekezwa katika kituo kikuu cha mabasi Jijini Mbeya mwishoni mwa mwaka jana amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa ngiri.

Mtoto huyo ambaye aliokotwa na mama lishe anayefahamika kwa jina la Subira Joseph Mwaijulu (Mama Sunche) mkazi wa Nonde Jijini Mbeya,ambaye amekuwa akimhudumia tangu alipotelekezwa amesema kuwa baada ya mtoto kuanza kusumbuliwa na ugonjwa huo aliamua kumpeleka Hospitali ya Rufaa kwa ajili ya matibabu.

Baada ya uchunguzi wa Madaktari walibaini mtoto Baraka Joseph(02) kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa ngiri hivyo waliamua kumfanyia upasuaji Machi 12 mwaka huu ambapo hivi sasa anaendelea vema na amelazwa wadi 6 ya watoto katika hospitali ya Rufaa na hali yake inaendelea vema.

Mama Sunche amemtaka mama aliyetelekeza mtoto huyo afike kumchukua kwani uwezo wake ni mdogo kiuchumi sasa shughuli zake zimekwama kutokana na muda mwingi kutumika kumhudumia mtoto pia kama mzazi wake aliona kuwa tatizo la ugonjwa ndiyo kikwazo asihofu kwani sasa mtoto ametibiwa.

Ametoa wito kwa wazazi na walezi kutowatelekeza watoto kutokana na ugumu wa maisha au mafarakano katika ndoa bali wanandoa watatue migogoro ya ndoa kwa hekima na uadilifu ili kupunguza wimbi la watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Baadhi ya mahitaji yanayohitajika kwa mtoto huyo na pamoja na nguo,chakula na mahitaji mengine madogo madogo kama sabuni na mafuta.

Aidha  amewaomba wasamaria wema kumsaidia chochote ili aweze kujikimu kimaisha kwani hakutarajia kupata mtoto kwa muda huu na Asasi zinazohudumia watoto kutokuwa na mwitikio wowote hivyo kuachiwa jukumu la kulea mtoto na ametoa wito mwenye kuguswa awasiliane nae kwa namba za simu 0753732025.

Vitendo vya kutelekeza watoto na unyanyasaji wa watoto ni miongoni mwa matukio yaliyoshika kasi hivi sasa katika mkoa wa Mbeya licha ya kuwepo kwa Taasisi nyingi zianazopiga vita zikiwemo TAMWA na TGNP.

Na Mbeya yetu