Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tunalaani vikali fujo na
uhabirifu wa mali unaofanywa na washabiki viwanjani wakati mechi
mbalimbali zikiwemo zile za kimataifa na ligi za hapa nchini.
Tunaiomba radhi Serikali kwa uharibifu wa viti uliotokea kwenye mechi
ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga ya Tanzania na Al Ahly ya
Misri iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Uharibifu huo wa viti umesababisha hasara ya sh. milioni 15 kwa
wamiliki wa uwanja huo ambao ni Serikali. TFF tutalipa fedha hizo kwa
Serikali kutokana na uharibifu huo.
Tunaendelea kuchunguza tukio hilo, huku tukijiandaa kutoa adhabu kwa
klabu na washabiki husika kulingana na kanuni zetu. Adhabu itakuwa kali
ili iwe fundisho kwa wengine.
Kwa mujibu wa Serikali, viti kumi viling’olewa na kutupwa ovyo ovyo
uwanjani wakati vingine 40 viliathirika kutokana na vurugu za watazamaji
hao.
Tumebeba dhamana ya kulipa uharibifu huo kwa vile TFF ndiyo wenye
dhamana ya kusimamia mechi za kimataifa, na ndiyo tulioomba idhini ya
kutumia uwanja huo.
Kwa vile sasa baadhi ya washabiki, wapenzi na wanachama wa klabu
mbalimbali nchini wanataka kufanya suala la uharibifu kuwa la kawaida na
mazoea, Serikali inakusudia kuchukua mapato yote ya mchezo husika
endapo kutatokea uharibifu.
Pia kuruhusu uwanja kutumiwa bila watazamaji kwa baadhi ya mechi, na
kutoruhusu uwanja huo kutotumika kabisa kwa baadhi ya mechi.
Boniface Wambura Mgoyo
Media and Communications Officer
Tanzania Football Federation (TFF)
0 comments:
Post a Comment