SAMSUNG CAMERA PICTURES
Wafanyakazi wanawake wa Airtel wakitoa huduma ya chakula kwa wafanyakazi wenzao wakati wa tafrija fupi waliyoiandaa kwa dhumuni la kukusanya fedha ili kuwachangia wagonjwa wa kansa waliopo hospitali ya Ocean Road jijini Dar es salaam.

SAMSUNG CAMERA PICTURES
Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil Colaso akichangia fedha kwa huduma ya Airtel Money kupitia simu wakati wa tafrija fupi iliyoandaliwa na umoja wa wanawake wa Airtel Tanzania kwa dhumuni la kuwachangia wanawake wanaosumbuliwa na maradhi ya kansa waliopo hospitali ya ocean road jijini Dar es salaam.
SAMSUNG CAMERA PICTURES
Mmoja kati ya wafanyakazi wa Airtel, Bw. Deodatus Hondo akichangia fedha wakati wa tafrija fupi iliyoandaliwa na umoja wa wanawake wa Airtel Tanzania kwa dhumuni la kuwachangia wanawake wanaosumbuliwa na maradhi ya kansa waliopo hospitali ya Ocean Road jijini Dar es salaam.
Umoja wa wafanyakazi wanawake wa Airtel Tanzania unaofahamika kwa jina la Airtel Divas leo wameandaa halfa ya kuchangisha pesa kwa ajili yakina mama  wanaosumbuliwa na maradhi ya kansa katika hospitali ya ocean road jijini Dar es salaam.
Halfa hiyo ya kuchangisha pesa ilifanyika katika makao makuu ya ofisi za Airtel Tanzania  na kushirikiksha wafanya kazi wa Airtel Tanzania kwa ujumla
Akizungumza kwa niaba ya  Airtel Ofisa Mahusiano na matukio Dangio Kaniki alisema” Airtel Tanzania kupitia Umoja wa wanawake Airtel Divas” tumeamua kuchangisha pesa kwaajili ya kina mama wenzetu ambao ni wagonjwa mahospitalini,  ambapo leo tumeaandaa kifungua kinywa kwa wafanyakazi wote wa Airtel na kiasi cha pesa kitakachopatikana kitaenda kusaidia wanawake wanaougua ugonjwa wa kansa katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Saalam.
Tunatambua jamii inayotuzunguka ina changamoto nyingi ikiwemo maradhi, na ndio sababu umoja wa wanawake wa Airtel tumeamua kuchangisha pesa kwa dhumuni la kuwasaidia wagonjwa hususani wakina mama wanaosumbuliwa na ugonjwa kansa. Tunaamini zoezi hili tunalolifanya leo litatuwezesha kufanikisha lengo letu.  Mpango huu wa kusaidia jamii zinazotuzunguka ni endelevu, na tumejipanga kutoa misaada ili  kuchangia katika kutatua vikwazo mbalimbali vya maisha na kujenga jamii iliyo bora. alisema Kaniki.
Kwa upande wa wafanyakazi Bi Doris Kibassa ambaye ni mmoja ya wanachama wa Airtel Diva alisema “ najisikia furaha kuwa sehemu ya kusaidia jamii,  mbali na kampuni yetu kuwa na shughuli za kijamii bado sisi  kama mfanyakazi tunanafasi ya kushiriki na kutoa msaada  kwa jamii. Tunaamini mchango huu tunaoutoa leo utaweza kunusuru maisha ya baadhi ya watanzania na hivyo basi tunaziasa asasi nyingine kuiga mfano huu  na kushiriki katika kuokoa maisha ya watanzania walio wengi,”
Airtel Tanzania imekuwa ikitoa michango kwa jamii kutupitia shughuli zake za huduma kwa jamii, Airtel kwa kushirikisha wafanyakazi wake pia inatoa huduma kwa jamii nchini.