Makamu
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe Samia Sululu Hassan akifungua
warsha ya siku moja kwa wahariri na waandishi wa habari juu ya nafasi
ya watetezi wa Haki za Binadamu katika Katiba mpya.
--
.waambiwa waache kamari ya majongoo kuhusu serikali mbili ama tatu
.watetezi wa haki za binadamu, waandishi watoswa kwenye rasimu ya Katiba
Na Damas Makangale, Dodoma, MOblog
WAANDISHI
na Wahariri wa vyombo vya habari nchini wamehimizwa kuzingatia maadili
ya uandishi wa habari na kuweka mbele maslahi ya taifa wakati wa
kuripoti Bunge maalum la katiba.
-
MOblog inaripoti.
Akifungua
warsha ya siku moja kwa waandishi wa habari kuhusu nafasi ya watetezi
wa haki za binadamu na asasi za kirai katika katiba mpya jijini Dodoma,
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe Samia Sululu Hassan
amesema waandishi wa habari wana nafasi kubwa ya kuelimisha jamii juu ya
haki za binadamu kupitia kalamu zao kwa kuzingatia weledi wa fani yao
na maadili ya uandishi.
“waandishi
wa habari pamoja na wahariri wao wanaweza kwa kuweka mbele maslahi ya
taifa kuripoti na kuandika habari zenye kuleta suluhu, amani, mshikamano
na utulivu,” amesema.
Mratibu
wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Ndg. Onesmo
Olengurumwa akitoa mada juu ya ya mtazamo na jukumu la wabunge wa katiba
na waandishi wa habari za katiba pamoja na watetezi wa haki za binadamu
katika mchakato wa kuandika Katiba mpya mkutano wa siku moja
uliofanyika mjini Dodoma.
Amesema
waandishi wa habari kwa kutumia kalamu zao wanaweza kushauri na
kushirikiana na serikali na mamlaka zingine kupatikana kwa katiba mpya
yenye tunu za taifa,
Sululu
aliongeza kwa kuweka hoja zao kwa ari ya utulivu wanaweza kabisa kuleta
mshikamano na ushirikiano wa kitaifa katika kudumisha amani na haki za
binadamu nchini.
Amesema
kwamba kupitia bunge la katiba wanahabari ni kiungo muhimu katika
kufikisha ujumbe kwa wananchi na kuelimisha umma jinsi sheria na haki za
binadamu zinavyoweza kulinda na katiba ya nchi.
Mwezeshaji, Mwandishi wa Habari, Mwanasheria, msomi na mjumbe wa Bunge la Katiba Ali Uki akizungumza kwenye warsha hiyo.
“waandishi
kwa kutumia nafasi yao wanaweza kushauri kwa kurekebishwa baadhi ya
sheria, vifungu ili kuweza kulinda haki za binadamu nchini kwa kupitia
bunge maalum la katiba,” aliongeza.
Alisisitiza
Mhe Sululu kwamba bunge la katiba halijadili kuhusu ama serikali mbili
au tatu kwa sababu kuna mambo mengi kwenye rasimu ya katiba
yakujadiliwa.
“kwa
jinsi mnavyoripoti kuhusu serikali mbili ama tatu ni kama mchezo wa
kamari ya majongoo jamani katiba siyo muungano tu,” amesema.
Kwa
upande, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC),
Onesmo olengurumwa amesema ingawaje kwenye rasimu ya katiba hawajatambua
watetezi wa haki za binadamu bali wataendelea kushauriana na wajumbe
kupata mwafaka wa jambo hilo.
Meza kuu, Ndg. Onesmo Olengurumwa akiwa na Mgeni rasmi Samia Suluhu Hassani kwenye warsha hiyo.
“Rasimu
ya katiba haijatambua mahali popote nafasi ya mashirika yasiyo ya
kiserikali yanayotetea haki mbali mbali za raia kama zilivyoanishwa
kikatiba,” amesema
Olengurumwa
aliongeza kwamba rasimu ya katiba pia haijatambua wasaidizi wa kisheria
wakujitolea (Paralegal) ambao wanatoa msaada mkubwa kisheria kwenye
ngazi za vijijini.
Amesema
ni muhimu kwa watanzania kuendelea kupanua mjadala wa katiba ili
misingi ya haki za binadamu iingie kwenye mifumo ya utetezi wa haki za
binadamu nchini.
Olengurumwa
amesema waandishi wa habari kama vile watetezi wa haki za binadamu
maisha yao lazima yalindwe na kutetewa na katiba ya nchi ili kujenga
mazingira mazuri ya haki za binadamu nchini.
Hivi
karibuni rasimu ya pili ya Katiba ilipendekeza Muungano wa Serikali
tatu – Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
na Serikali ya Tanganyika.
Mjadala
wake ulianza, ambapo wasomi walikosoa takwimu za Tume ya Mabadiliko ya
Katiba kuhusu idadi ya waliotoa maoni, kuwa zimetumika kuupotosha umma.
wahadhiri
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sabato Nyamsenda na Bashiru Ally
wakati wakizungumza katika kipindi cha Je, Tutafika? kinachorushwa na
Channel Ten hivi karibuni.
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo waandishi na wahariri kutoka vyombo mbalimbali nchini.
Nyamsenda
amesema ukweli wa takwimu hizo uko kwenye ripoti ya Tume hiyo, ambayo
haipatikani kwa urahisi huku watu wakiishia tu kusoma tu rasimu ambayo
haielezi majukumu waliyopewa, mahali walipopita, idadi ya wananchi na
maoni yao.
Takwimu za Tume
Akifafanua
zaidi, Nyamsenda anasema takwimu zinazotajwa kwamba asilimia 61 ya
Watanzania Bara wanataka Serikali tatu, asilimia 60 ya Wazanzibari
wanataka Serikali ya Mkataba si za kweli.
“Tume
ya Warioba imetoa takwimu kuwa, watu waliotoa maoni kwa jumla ni
333,537. Kati yao, waliogusia Muungano ni 77,000, kwa hiyo 256,537
hawakugusia Muungano,” anasema na kuongeza:
“Ukiwagawanya
katika Bara utakuta ni watu wapatao 36,000 na Visiwani watu 38,000.
Kati ya waliozungumzia muungano. Kwa Zanzibar watu 19,000 hawakugusia
muundo na watu 10,400 ndiyo waligusia Muungano wa Mkataba.”
Anaendelea
kufafanua: “Waliozungumzia Serikali mbili ni 6,460 sawa na asilimia 34.
Kwa hiyo ni wachache kuliko waliozungumzia Serikali ya Mkataba ambao
nao ni wachache kuliko wale ambao hawakugusia kabisa suala la muungano.
Ni sawa na tone la maji katika bahari,” amesema.
Benedict Ishabakaki, Afisa Usalama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu akishiriki mkutano huo.
Anaendelea kufafanua kuwa waliotoa maoni kuhusu Serikali ya Mkataba na Serikali tatu, ni wachache huku wengi wakiwa Bara.
“Kama
jumla ya watu waliotoa maoni ya Katiba ni 333,537, huwezi ukachukua
watu 16,000 waliotaka Serikali tatu ukawaziba wengi ambao hawakutaka,”
anasema na kuongeza:
“Ukijumlisha
watu wanaotaka Serikali moja na mbili ambao ni 16,475, utaona ni wengi
kuliko wanaotaka Serikali tatu ambao ni 16,470.”
Anasema watu hao wakiwekwa katika kundi ambalo halikugusia kabisa muundo wa muungano, ni watu 287,537 sawa na asilimia 86.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo ya siku moja.