Baadhi ya wajumbe wa bodi ya Dawasa wakisikiliza
Baadhi
ya wataalamu wa washauri miradi mitatu inayotakiwa kutekelezwa ya
ujenzi wa Bwawa la Kidunda wakwemo wa kutoka nje ya nchi wakijandaa
kuwasilisha ripoti ya utafiti wa miradi hiyo kwa wadau.
Baadhi
ya watendaji wa wizara ya maji pamoja na Mamlaka za Dawasa na Dawasco
katika picha ya pamoja na viongozi wakuu wakwemo wakuu wa Mikoa ya Moro,
Pwani na Dar es salaam
Hakuna kulala katika kupata picha za kumbukumbu.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kushoto) akisalimana na mwezake wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadiki.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadiki akitoa maelezo machache kuhusu suala la upatikanaji wa maji Mkoani mwake.
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani, Mwatumu Mahiza , akitoa salamu pamoja na umuhimu wa
ushirikishwaji wadau mbalimbali katika kulinda mazingira na vyanzo vya
maji.
Viongozi wa juu wa Dawasa wakiteta jambo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Kibena Kingo ( kulia ) akimsikiliza mwezake kabla ya kuanza kwa warsha.
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani, Mwatumu Mahiza ( kushoto) akisalimana na mwezake wa
Dar es Salaam, Mhe Saidi Mecky Sadiki na aliyekati kati ni Mkuu wa
Wilaya ya Morogoro, Said Amanzi.
Baadhi
ya wadau wa Vijij vya Kidunda, wakiwa kwenye picha ya pamoja na
Viongozi wa juu wa Serikali kutika Wizara ya Maji, Dawasa na wakuu wa
mikoa ya Moro, Dsm na Pwani.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Dawasa kwenye
picha ya pamoja na Viongozi wa serikali
Baadhi ya wajumbe wa bodi ya Dawasa wakisikiliza
hotuba ya mgeni rasmi. Picha na John Nditi
=====*****=====
Na John Nditi, Morogoro
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro, Dk Joel Bendera amefungua warsha ya wadau
kujadili taarifa ya tathimini ya athari za kijamii na mazingira ya mradi
wa ujenzi wa barabara ya Ngerengere hadi Kidunda kwa kiwango cha
changarawe, ujenzi wa mtambo mdogo wa kufua umeme wa megawati 20 na njia
ya umeme kutoka Kidunda hadi Chalinze.
Dk
Bendera amezindua warsha hiyo katika ukumbi wa hoteli ya Nashera ya
Mjini Morogoro , kwa niaba ya Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe.
Warsha
hiyo ya siku moja pia ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe
Mwatumu Mahiza, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Saidi Mecky Sadiki,
wabunge wa Mkoa wa Morogoro akiwemo wa Jimbo la Morogoro Kusini,I
nnocent Kalongeries , na Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Mhe Said Amanzi na
wawakilishi wa makundi mengine 14 likiwemo la viongozi wa wananchi wa
vijiji na kata zinazopitiwa na miradi hiyo.
Kwa
mujibu wa hotuba ya Waziri huyo iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,
kuwa wazo la kujenga bwawa la Kidunda kwa ajil ya matumzi mbalimbali
ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za maji ya Jiji la Dar es Salaam ,
lililokuwepo muda mrefu.
Hivyo
alisema kukamilika na kuanza kutumika kwa barabara na mtambo mdogo wa
umeme na hatimaye ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme huo kutoka
Kidunda hadi kituo cha umeme chalinze , kutatoa fursa mbalimbali za
kuchumi na kijamii katika maeneo ya mradi huo.