SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Saturday, March 15, 2014

Rais Jakaya Kikwete na Viongozi wa Bunge Maalum la Katiba IKULU Ndogo Mjini Dodoma Muda mfupi baada ya Kuwaapisha

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mh.Samuel Sitta(kushoto) na Makamu Mwenyekiti Mhe.Samia Suluhu(kulia) wakati wa hafla  ya kuwaapisha katibu na naibu katibu wa Benge maalum la katiba zilizofanyika katika viwanja vya ikulu ndogo mjini Dodoma jana asubuhi
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Katibu na naibu katibu wa Bunge maalum la Katiba muda mfupi baada ya kuwaapisha katika ikulu ndogo mjini Dodoma jana  asubuhi.Kushoto ni Katbu Wa Bunge hilo Bwana Yahya Khamis Hamad na kulia ni Naibu Katibu Dkt.Thomas Kashililah.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa serikali na viongozi wa bunge maalum la katiba muda mfupi baada ya kuwaapisha Katibu na Naibu Katibu wa Bunge hilo katika hafla iliyofanyika ikulu ndogo mjini Dodoma jana . Kutoka kushoto ni Katibu wa Bunge maalum la Katiba Bwana Yahya Khamis Hamad,Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue. Waziri Mkuu Mizengo Pinda ,Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mh.Samuel Sitta,Makamu Mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba Mh.Samia Suluhu, Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Sefu Iddi, Naibu Katibu wa Bunge Maalum Dkt.Thomas Kashilila na kulia ni Mwenyekiti wa muda wa Bunge maalum la katiba aliyemaliza muda wake Mh.Pandu Ameir Kificho(picha na Freddy Maro).
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifurahi  jamabo na viongozi waandamizi wa serikali na viongozi wa bunge maalum la katiba muda mfupi baada ya kuwaapisha Katibu na Naibu Katibu wa Bunge hilo katika hafla iliyofanyika ikulu ndogo mjini Dodoma jana . Picha na Freddy Maro-IKULU