Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipokea toka kwa Kamishna wa Sensa Hajjat
Amina Mrisho Ripoti ya Mgawanyo wa Watu kwa Umri na Jinsia kwa data za
sensa ya watu na makazi mwaka 2012 leo Machi 13, 2014 Ikulu jijini Dar
es salaam.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Kamishna wa Sensa Hajjat Amina Mrisho
(kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina
Chuwa baada ya kupokea Ripoti ya Mgawanyo wa Watu kwa Umri na Jinsia
kwa data za sensa ya watu na makazi mwaka 2012 leo Machi 13, 2014
Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu Dkt. Albina Chuwa ambaye pamoja na Kamishna wa Sensa Hajjat
Amina Mrisho baada ya kupokea Ripoti ya Mgawanyo wa Watu kwa Umri na
Jinsia kwa data za sensa ya watu na makazi mwaka 2012 leo Machi 13,
2014 Ikulu jijini Dar es salaam.(Picha na IKULU).
Piramidi
ya Idadi ya Watu nchini Tanzania inaonesha kuwa idadi kubwa ya watu
hapa nchini ni watoto wenye umri wa chini ya miaka 15 na vijana.
Asilimia
44 ya watu wote hapa nchini ni watoto wenye umri chini ya miaka 15,
ambapo utafiti wa Mama na Mtoto wa Mwaka 2010 unaonesha kuwa kiwango cha
uzazi ni wastani wa watoto 5.4 kwa kila mama mwenye umri wa kuzaa
ambao ni miaka 15-49.
Sera ya Vijana Tanzania ya Mwaka 2007 inatambua Vijana kuwa ni watu
wote wenye umri wa miaka 15-35, ambapo kulingana na Sensa ya Mwaka 2012
ni asilimia 34.7 ya watu wote hapa nchini.
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dk. Albina Chuwa amemueleza Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo
Ikulu wakati akimkabidhi vitabu na majedwali yenye matokeo na machapisho
ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012.
Kulingana
na Takwimu, idadi ya watu Tanzania imeongezeka zaidi ya mara tatu
kutoka watu Milioni 12.3 kwa Mwaka 1967 hadi watu milioni 44.9 Mwaka
2012.
Takwimu
hizo zinaonesha kuwa Mkoa wa Dar es Salaam una asilimia kubwa ya Vijana
wenye umri wa miaka 15-35 wakati Mkoa wa Singida ukiwa na asilimia
ndogo zaidi.
Kulingana
na Takwimu, zaidi ya nusu ambayo ni asilimia 52.2 ya watu wote nchini,
wako katika umri wa kufanya kazi ambapo Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza
kwa kuwa na asilimia kubwa ya watu wenye umri huu wa kufanya kazi na
Mkoa wa Simiyu uko chini zaidi kwa kuwa na asilimia 45.5 ya watu hawa.
Katika takwimu hizo, zaidi ya nusu ya watu katika Mikoa ya Simiyu, Rukwa na Geita ni Watoto wenye umri wa chini ya miaka 15.
Dk.
Chuwa pia amebainisha kuwa Takwimu zinaonesha kuwa rasilimali watu kwa
ajili ya kuzalisha na kuongeza Uchumi na kupunguza Umaskini sio tatizo
hapa nchini na kinachotakiwa ni watu wote kutumia fursa zilizopo nchini
kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kuinua uchumi wa Nchi.
Kulingana
na takwimu asilimia 5.6 ya watu hapa nchini ni wazee na takwimu hizi
zinaonesha kuwa wazee kwa asilimia kubwa wako katika Mikoa ya
Kilimanjaro, Mtwara, Lindi na Pwani ambapo asilimia ndogo zaidi wapo
katika Mikoa ya Dar es Salaam na Mjini Magharibi. Kwa mujibu wa Sera ya
wazee Tanzania, Mzee ni mtu mwenye umri wa miaka 60 au zaidi.
Takwimu
pia zinazidi kuonesha kuwa asilimia ya watu wanaoishi Mijini
imeongezeka zaidi ya mara tano ambapo ni asilimia 6.4 mwaka 1967 na
kufikia asilimia 29.6 kwa mwaka 2012.
Jiji
la Dar es Salaam lina asilimia 10 ya watu wote hapa Tanzania Bara
wakati Mjini Magharibi ina asilimia 46 ya watu wote wa Zanzibar.
Sensa
pia imeonesha kuwa Wanawake ni wengi zaidi , kwa asilimia 51
ukilinganisha na wanaume ambao ni asilimia 49 kama ilivyo katika nchi
nyingi Barani Afrika.
Hapa
Tanzania Mkoa wa Manyara unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya Wanaume
ambapo Mkoa wa Njombe una idadi ndogo zaidi ya wanaume.