Mabere Nyaucho Marando akiongea na waandishi wa Global Publishers (hawapo pichani).
====****====
Na Elvan Stambuli
WAKILI maarufu nchini, Mabere Nyaucho Marando amesema mwanamuziki Nguza Viking ‘Babu Seya’ na watoto wake watatu walimbambikiwa kesi.
WAKILI maarufu nchini, Mabere Nyaucho Marando amesema mwanamuziki Nguza Viking ‘Babu Seya’ na watoto wake watatu walimbambikiwa kesi.
Akizungumza na waandishi wa habari wa Global Publishers katika ofisi
zao zilizopo Mwenge Bamaga mwishoni mwa wiki iliyopita, Marando alisema
alipitia jalada la kesi hiyo lenye kurasa 1,362 na kugundua kuwa hakuna
hata sehemu moja inayomhusisha kigogo mmoja wa nchi, lakini kesi
walikuwa wamebambikiwa.
Hakutaja waliombambikia. Baadhi ya mahojiano ya Marando na waandishi wetu yalikuwa kama ifuatavyo:
Mwandishi: Wewe uliwatetea Babu Seya na watoto wake, unaweza kutueleza ilikuwaje ukatafutwa wewe kuwatetea?
Mwandishi: Wewe uliwatetea Babu Seya na watoto wake, unaweza kutueleza ilikuwaje ukatafutwa wewe kuwatetea?
Marando: Kuna rafiki yangu alikuja kuniomba nifanye kazi ile,
nilikataa hasa kwa kuwa nami nina watoto wa kike. Baadaye nilikubali
kwanza kusoma jalada la kesi lenye kurasa 1,362 nikaona hawakufanya
makosa waliyoshitakiwa, walibambikiwa nikaamua kuwatetea katika ngazi ya
rufaa, niliwatetea bure kabisa.
Mwandishi: Kama hivyo ndivyo, ina maana makosa walibambikiwa?
Mwandishi: Kama hivyo ndivyo, ina maana makosa walibambikiwa?
Marando: Ndiyo, naamini makosa yale walibambikiwa lakini siyo na
kigogo yeyote wa serikali katika nchi hii. Lakini Mahakama ya Rufaa
haina makosa, Babu Seya na wanawe walikuwa wamehukumiwa na magazeti.
Nyinyi waandishi mlimhukumu kwa hii fabricated case (kesi ya kutunga) na
sababu zipo.
Mwandishi: Je, kuna njia yoyote iliyobaki ya kumtoa Babu Seya na mwanaye?
Mwandishi: Je, kuna njia yoyote iliyobaki ya kumtoa Babu Seya na mwanaye?
Marando: Mimi kama wakili, hapo ndiyo mwisho wangu, nimenyoosha
mikono. Nimeshindwa nusu, nimeshinda nusu (Kwa kuwatoa jela Mbangu na
mdogo wake Francis Nguza na kubaki jela Nguza na Papii.)
Mwandishi: Umekuwa Chadema na kuna habari kuwa uliondolewa kuwa
mwanasheria wa chama akapewa Tundu Lissu,pia kuna habari kuwa umekosana
na mwenyekiti wako, Freeman Mbowe, Je, kuna ukweli wowote juu ya hayo?
Marando: Sijawahi kuwa mwanasheria wa Chadema isipokuwa wanapokuwa na
tatizo la kisheria huwa nawapa ushauri wakihitaji. Mheshimiwa Mbowe
sijakosana naye isipokuwa katika vikao tunaweza kutofautiana na hivyo
ndivyo chama makini kilivyo. Wote hamuwezi kuwa na wazo moja katika
hoja, baadaye inapigwa kura, upande unaoshinda na unaoshindwa huwa kitu
kimoja. Hakuna ugomvi hapo, mimi ni Makamu Mwenyekiti Kanda ya Pwani na
Mjumbe wa Kamati Kuu.
Mwandishi: Lipo suala kuwa wewe ni usalama wa taifa na ulihusika na mauaji ya Komandoo Tamim, Je, hilo unaweza kulifafanua?
Marando: Mimi nilijiunga na usalama wa taifa na nilikuwa kitengo cha
mambo ya nje hasa kuhusu vyama vya ukombozi enzi hizo. Niliacha kazi
hiyo kwa kukabidhi barua kwa aliyekuwa mkurugenzi wake, Dk. Hansy Kitime
baada ya kulazimishwa kujiunga na TANU kwani sikuwa mwanachama. Kuhusu
Tamim aliuawa mwaka 1983 wakati huo mimi nilikuwa nimeshaacha kazi.
Hili la kuua walikuwa wakinipakazia watu wa usalama wa taifa bila
shaka kwa sababu niliacha kazi kijeuri nikawa jobless (sina kazi).
Baadaye nikaajiriwa Shirika la Sheria Tanzania kabla ya kuanzisha
kampuni yangu ya uwakili mwaka 1984. Nimefafanua hili mara nyingi sana,
nadhani leo mmenielewa na Watanzania watanielewa.
CHANZO:NA GPL
0 comments:
Post a Comment