Maofisa hao ni Naibu Katibu Mkuu (Fedha na
Utawala), Jean-Claude Nsengiyiyumva anayetuhumiwa kujichotea malipo ya
posho ya vikao kwa kujiandika kwenye orodha ya washiriki wa vikao vitatu
tofauti vinavyofanyika kwa wakati mmoja bila kuhudhuria na Ofisa Milki
Mwandamizi, Phil Klerruu anayetuhumiwa kuchukua mali za jumuiya kinyume
cha sheria.
Wakizungumzia tuhuma dhidi yao kwa nyakati
tofauti, Nsengiyumva na Klerruu walikana huku kila mmoja akimtuhumu
mwenzake kuratibu mikakati ya kumchafua mwenzake.
“Sina hofu na tuhuma zinazoelekezwa dhidi yangu kwa sababu
hazina ukweli. Nimesikia SG (Katibu Mkuu), ameunda kamati kunichunguza
ingawa sina taarifa rasmi. Ngoja tusubiri kwa sababu ukweli wote
utadhihirika,” alisema Nsengiyumva.
Naibu Katibu Mkuu huyo anadaiwa kumtumia Katibu
Muhtasi wake, Caroline Mudambo kumsainia katika orodha ya washiriki wa
vikao ambavyo hakuhudhuria.
Nsengiyumva ambaye amekuwa katika wadhifa huo kwa
miaka mitano tangu alipoteuliwa na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi
mwaka 2009, pia anatuhumiwa kugoma kuidhinisha mikataba mipya ya baadhi
ya wafanyakazi kutokana na chuki na masuala binafsi.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea.....
0 comments:
Post a Comment