Utawala
wa jimbo Colorado nchini Marekani,umesema kuwa katika kipindi cha siku
za kwanza thelathini tangu ukuzaji na uuzaji wa bangi kuhalalisha,
umekusanya zaidi ya dola milioni mbili kama ushuru.
Jimbo hilo ndilo eneo la kwanza duniani kuwahi kuhalalisha uuzaji wa bangi kwa matumizi wa starehe.
Kwa
mujibu wa takwimu bangi inayokisiwa kugharimu dola milioni kumi na nne
iliuzwa mwezi Januari, wakati sheria hiyo ilipoanza kutekelezwa.
Ruhusa
uuzaji wa bangi na ushuru utaongezeka maradufu, ni moja kati ya masuala
yaliyopogiwa debe na wanaharakati wanaunga mkono matumizi ya bangi
katika jimbo Colorado.
Watu wakivuta bangi Colorado
Na ikiwa
takwimu za uuzaji huo katika mwezi wa kwanza ni za kuaminika, basi
utawala wa jimbo hilo unajiandaa kupokea fedha zaidi za matumizi kutoka
na ulevi huo wenye utata.
Bangi yenye dhamani ya dola milioni kumi na nne iliuzwa Januari pekee, wakati sheria hiyo ilioidhinishwa
Wapiga
kura waliidhinisha sheria hiyo baada ya kura ya maoni katika majimbo ya
Colorado na Washington licha ya kuwa serikali ya Marekani, ingali
imeorodhesha bangi kama dawa ya kulevya.
Jimbo la Colorado, ilikuwa jimbo la kwanza kuruhusu maduka kuuza bangi na inatoza ushuru wa uugizaji na uuzaji.
Bangi inayouzwa Colorado
Kuambatana na sheria hiyo dola milioni arubaini ya kwanza itakayokusanywa kama ushuru itatumiwa kujenga shule zaidi.
Hata
hivyo bado kuna mjadala mkali si tu kuhusu swala hilo nyeti la kuruhusu
uzwaji bangi, lakini pia khusu ni mradi upi utafadhiliwa baada ya mradi
huo wa ujenzi wa shule kukamilika .
Baadhi ya
raia nao wanataka fedha hizo kutumiwa kuthibiti uuzaji na ukuzaji wa
bangi nao wengine wakipendekeza kutumiwa kwa kampeini ya kuwahimiza
watoto kutojiingiza katika tabia ya uvutaji bangi na pia kupigia debe
kampeni ya kuwashawishi watu wasiendeshe gari wakiwa wamevuta bangi.
Na BBC
Swahili
0 comments:
Post a Comment