SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, March 17, 2014

CCM YASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE JIMBO LA KALENGA


Mgombea Ubunge Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Godfrey Mgimwa  akiwa amebebwa na wafuasi wa chama hicho jana usiku katika Ofisi ya CCM Mkoa wa Iringa baada kutangazwa matokeo ya awali yasiyo rasmi .Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka na ushindi wa kishindo kwa kushinda kata zote 13 zilizoko kwenye jimbo hilo la Kalenga

Matokeo ya Uchaguzi Mdogo jimbo la Kalenga Iringa vijijini yametangazwa rasmi jana usiku na Tume ya Taifa ya Uchaguzi mjini Iringa,kuwa chama cha CCM kilipata jumla ya kura 22962,na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Kilipada idadi ya jumla kura 5853 na chama cha CHAUSTA kilipata kura 150.Hivyo chama cha CCM kilishinda kwa asilimia 79.4,CHADEMA asilimia 20.1 na CHAUSTA asilimia 0.5.Matokeo hayo ni ya jumla kwa Kata 13 za jimbo hilo