Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya sherehe za Maulid kwa
wanawake wa mkoa wa Dar es salaam, kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume
Muhammad (S.W.A), Aisha Sururu (wa pili kushoto), akifuatilia jambo
Kikundi cha kaswida kutoka madrasa ya Al Itiswam, Sokota
Temeke Dar es Salaam, ikisherehesha katika sherehe hizo.
Mtoa mada ihusuyo elimu ya kiislam na mwanamke, Atwiya Adam Ahmad, akieleza ujumbe muhimu kuhusu kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), na umuhimu wa kuadhimisha siku hiyo.
Kikundi cha kaswida kutoka madrasa ya Al Itiswam, Sokota
Temeke Dar es Salaam, ikisherehesha katika sherehe hizo.
==****==
WANAWAKE nchini wametakiwa kujiamini sambamba na kuwalea watoto katika maadili mema ili kuzuia mmomonyoko wa maadili ambao ni chanzo cha uhalifu nchini.
Mwanaharakati wa Kiislam na diwani wa viti maalum kwa tiketi ya Chama
cha Mapinduzi Ilala,Aisha Sururu aliyasema hayo jijini Dar es salaam
wakati wa maadhimisho ya Maulid ya kuzalima Mtume, Muhammad(S.A.W), yaliyoandaliwa na wanawake wa mkoa huo.
"Kinamama na jamii nzima ya Kiislam sote tunapaswa tuwe wakuzi wazuri
wa watoto wetu ilu kuzuia mmomonyoko wa maadili" alisema.
Alisema wao kama wanawake wameamua kusherehekea mazazi ya Mtume kwa kuwa kabla ya kuzaliwa mtume wanawake walidhalilishwa sana, lakini kwa kipindi chake wanawake walipewa nafasi kubwa.
"Zamani wanawake tulinyanyaswa na kudhalilishwa sana ila enzi ya Mtume
Mohamad ndo tukapewa nafasi. Hivyo wanawanke tuko mbele toka enzi ya
mtume" alisema.
Aliwataka wanawake kujiamini kwamba wanaweza katika mikakati yoyote ya maendeleo kwa kuwa wanatambulika tangu enzi za mtume.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa baraza hilo, Mayasa Sadala
aliitaka jamii kufuata taratibu za mtume alizoziacha ikiwemo stara ili
kuendelea kuidumisha amani na utulivu.
0 comments:
Post a Comment