Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es
Salaam, Suleiman Kova akiwaonyesha waandishi wa habari mapanga
waliyoyakamata wakati wa msako mkali wa kuwasaka watuhumiwa waliomvamia na
kumshambulia Dk Sengondo Mvungi Mjumbe wa Tume ya Katiba. Katika msakao huo
watuhumiwa tisa walikamatwa wakiwa na mapanga na simu moja ya mkononi. Katikati
(waliokaa meza kuu) ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi.
Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Hata hivyo, Waziri
Nchimbi aliwaomba wananchi na waandishi wa habari wawe na subira wakati Jeshi la
Polisi likiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata watuhumiwa wengine.
Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, jijini Dar es Salaam jana
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na tukio la kuvamiwa na kushambuliwa Dk Sengondo Mvungi, Mjumbe wa
Tume ya Katiba. Waziri Nchimbi alisema upepelezi wa tukio hilo umefanikiwa kwa
zaidi ya asilimia 80 ambapo tayari watuhumiwa tisa wamekamatwa wakiwa na mapanga
na simu moja ya mkononi, watuhumiwa hao walitajwa majina yao katika mkutano huo
uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es
Salaam jana. Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaomba wananchi na waandishi wa
habari wawe na subira wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kwa ajili
ya kuwakamata watuhumiwa wengine. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo,
Pereira Ame Silima. Kulia ni Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam,
Suleiman Kova.
Sehemu ya
waandishi habari waliohudhuria mkutano wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alipokuwa anazungumza na waandishi wa vyombo
mbalimbali vya habari vya nchini na nje ya nchi kuhusiana na tukio la kuvamiwa
na kushambuliwa Dk Sengondo Mvungi, Mjumbe wa Tume ya Katiba. Waziri Nchimbi
alisema upepelezi wa tukio hilo umefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 80 ambapo
tayari watuhumiwa tisa wamekamatwa wakiwa na mapanga na simu moja ya mkononi,
watuhumiwa hao walitajwa majina yao katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam jana. Hata hivyo,
Waziri Nchimbi aliwaomba wananchi na waandishi wa habari wawe na subira wakati
Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata watuhumiwa
wengine.
Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
0 comments:
Post a Comment