SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, November 12, 2013

MH BALOZI BATILDA AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO KWA RAIS WA SEYCHELLES

MheshimiwaBalozi Batilda S. Burian, Baloziwa Tanzania nchini Seychelles mwenye makazi yake nchini Kenya, aliwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mheshimiwa James Alix Michel, Rais wa Jamhuri ya Seychelles tarehe 5 Novemba, 2013 katika Ikuluya Rais Seychelles.

 Hafla ya kuwasilisha hati hizo, imefungua ukurasa mpya wa mashirikiano kati ya nchi hizi mbili. Takriban kwa kipindi cha zaidi ya miaka 15 hatukuwahi kuwa na Balozi aliyewahi kuwasilisha Hati zaUtambulisho nchini Seychelles. Mh. Balozi alifuatana na Brig. Gen. E.V. Milinga, Mwambata Jeshi, Ubalozi wa Tanzania Nairobi

Katika hafla hiyo ,Mheshimiwa Balozi alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Rais James A. Michel, mazungumzo ambayo yalilenga zaidi katika biashara, uwekezaji, mashirikiano ya anga usafiri wa majini, ulinzi na usalama. 

Pia Mheshimiw Balozi Burian alipata fursa ya kuona  na na mawaziri wafuatao na kufanya nao mazungumzo:-
(i)               Mheshimiwa Prof. RolphPayet, WaziriwaMazingira naNishati
(ii)            Mheshimiwa Christian Lionnet, Waziri wa Ardhi naNyumba
(iii)         Mheshimiwa Pierre Laporte, Waziri waFedha
(iv)          Mheshimiwa Dkt Patrick S. Herminie, Spikawa Bunge
(v)             Bib iBenjamine Rose, KatibuMkuu, WizarayaUtalii naUtamaduni.

Ubaloziwa Tanzania Nchni Kenya pia unawakilisha nchi za Sudani, SudaniKusini, Somalia, Eritrea na Djibouti.
MheshimiwaBalozi Batilda S. Burian, Baloziwa Tanzania nchini Seychelles mwenye makazi yake nchini Kenya, aliwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mheshimiwa James Alix Michel, Rais wa Jamhuri ya Seychelles tarehe 5 Novemba, 2013 katika Ikuluya Rais Seychelles.
Mh. Rais James Alix Michel wa Seychelles akiwa katika mazungumzo na MheshimiwaBalozi Batilda S. Burian mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho. Mazungumzo hayo yalilenga zaidi katika Mashirikiano ya kiuchumi kati ya nchi hizi mbili.
Mh. Rais James Alix Michel wa Seychelles akiwa katika picha ya pamoja na na MheshimiwaBalozi Batilda S. Burian. Kulia kwa Mh. Rais Michel ni Brig. Gen. E.V. Milinga, Mwambata Jeshi, Ubalozi wa Tanzania, Nairobi Kenya.
Mh. Balozi Batilda Burian akiwa katika mazunguzo na Mheshimiwa Prof. Rolph Payet, WaziriwaMazingira naNishati.
Mh. Balozi Batilda Burian akiwa katika mazunguzo na Mheshimiwa Christian Lionnet, WaziriwaArdhi na Nyumba. Mazungumzo hayo yalihusu namna ya kuimarisha mahusiano yetu katika sekta ya ardhi na nyumba.
Mh. Balozi Batilda Burian akiwa katika mazunguzo Mheshimiwa Pierre Laporte, Waziri wa Fedha.
Mh. Balozi Batilda Burian akiwa katika mazunguzo na Mheshimiwa Dkt Patrick S. Herminie, Spikawa Bunge la Jamhuri ya Seychelles.

NA ANKAL ISSA MICHUZI
 

0 comments:

Post a Comment