SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.
Showing posts with label DK SENGONDO MVUNGI. Show all posts
Showing posts with label DK SENGONDO MVUNGI. Show all posts

Tuesday, November 12, 2013

SERIKALI YAWAKAMATA WATUHUMIWA TISA TUKIO LA KUVAMIWA NA KUSHAMBULIWA MJUMBE WA TUME YA KATIBA, DK SENGONDO MVUNGI

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova akiwaonyesha waandishi wa habari mapanga waliyoyakamata wakati wa msako mkali wa kuwasaka watuhumiwa waliomvamia na kumshambulia Dk Sengondo Mvungi Mjumbe wa Tume ya Katiba. Katika msakao huo watuhumiwa tisa walikamatwa wakiwa na mapanga na simu moja ya mkononi. Katikati (waliokaa meza kuu) ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaomba wananchi na waandishi wa habari wawe na subira wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata watuhumiwa wengine. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam jana