Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuashiria
kuweka Jiwe la Msingi katika benki ya Maendeleo PLC, wakati wa hafla ya uzinduzi
rasmi wa benki hiyo, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Askofu Mkuu
wa Kanisa la KKKT, Dkt. Alex Malasusa (kushoto) ni Naibu Waziri wa Fedha,Janeth
Mbene.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria
kufungua benki ya Maendeleo PLC, wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa benki
hiyo, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la
KKKT, Dkt. Alex Malasusa (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck
Sadic na Naibu Waziri wa Fedha,Janeth Mbene.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi mfano wa kadi
ya ATM, mteja wa kwanza kufungua Account katika benki hiyo, Elianasa Marco
Njiu,mkazi wa jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Benki hiyo
iliyofanyika jijini Dar es Salaam, leo Nov 12, 2013. Wa pili (kulia) ni Mteja wa
kwanza kupata mkopo katika benki hiyo, Margareth Chiwata.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti,
Mchungaji, George Fupe, ambaye ni mmoja kati ya waanzilishi wa benki hiyo na
wahamasishaji kwa watu kununua shea katika benki hiyo, ambapo walifanikiwa
kupata jumla ya Sh. Bilioni 4.5. Makamu alikabidhi vyeti hivyo wakati wa hafla
ya uzinduzi rasmi wa benki hiyo iliyopo jijini Dar es Salaa,leo Nov 12, 2013.
Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dkt. Alex Malasusa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa
ufunguzi rasmi wa bemki hiyo,leo.
Sehemu ya wageni waalikwa
waliohudhuria hafla hiyo ya ufunguzi wa benki hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo na wachungaji wa Kanisa la KKKT,
baada ya ufunguzi rasmi wa benki hiyo.
Picha na OMR
0 comments:
Post a Comment