SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.
Showing posts with label JIJINI DAR LEO. Show all posts
Showing posts with label JIJINI DAR LEO. Show all posts

Wednesday, February 12, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA TAFAKURI MARIDHIANO KUELEKEA KATIBA MPYA, JIJINI DAR LEO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Kongamano la Tafakuri na Maridhiano kuelekea Katiba mpya, lililofanyika kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam, leo Feb 12, 2014 na kushirikisha Vyama vya Siasa, Makundi ya dini na Asasi za kiraia. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, baada ya kufunguliwa rasmi rasmi Kongamano la Tafakuri na Maridhiano kuelekea Katiba mpya, lililofanyika kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam, leo Feb 12, 2014 na kushirikisha Vyama vya Siasa, Makundi ya dini na Asasi za kiraia. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiagana na wajumbe walioshiriki Kongamano hilo baada ya ufunguzi uliofanyika kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam leo Feb 12, 2014 na kushirikisha Vyama vya Siasa, Makundi ya dini na Asasi za kiraia. Picha na OMR

Picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo.

Wednesday, November 13, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA TAMASHA LA 11 KWA ASASI ZA KIRAIA, JIJINI DAR LEO

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia washiriki wa Tamasha la 11 la Asasi za Kiraia, wakati alipokuwa akifungua rasmi Tamasha hilo katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam

Tuesday, November 12, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA RASMI BENKI YA MAENDELEO PLC, JIJINI DAR LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuashiria kuweka Jiwe la Msingi katika benki ya Maendeleo PLC, wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa benki hiyo, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dkt. Alex Malasusa (kushoto) ni Naibu Waziri wa Fedha,Janeth Mbene.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kufungua benki ya Maendeleo PLC, wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa benki hiyo, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dkt. Alex Malasusa (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadic na Naibu Waziri wa Fedha,Janeth Mbene

Wednesday, October 23, 2013

Makamu wa Rais Dkt. Bilal afungua Kongamano na Maonyesho ya pili ya siku mbili ya Mafuta na Gesi, Jijini Dar leo

01
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano na maonyesho ya pili ya siku mbili ya Mafuta na Gesi, yaliyoanza leo kwenye Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 (Picha zote na OMR).

Tuesday, May 21, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA 14 WA BARAZA LA USIMAMIZI WA MAWASILIANO AFRIKA, JIJINI DAR LEO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Mkutano wa 14 wa baraza la usimamizi wa Mawasiliano Afrika, uliofunguliwa leo Mei 21, 2013 kwenye Hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka nchi za Afrika, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akifungua rasmi mkutano huo wa 14 wa baraza la usimamizi wa Mawasiliano Afrika, uliofunguliwa leo Mei 21, 2013 kwenye Hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongoza na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Prof. John Mkoma, wakati akiondoka kwenye chumba cha mkutano baada ya kufungu rasmi mkutano huo wa 14 wa baraza la usimamizi wa Mawasiliano Afrika, uliofunguliwa leo Mei 21, 2013 kwenye Hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya washiriki wa mkutano huo, baada ya ufunguzi.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.