Ofisa
Mtendaji wa Kata ya Gongo la Mboto Bw. Alphonce Msenduki akisoma taarifa
ya kiwanda cha kuchambua taka (KIKUTA) mbele ya mgeni rasmi Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa alipotembelea
kiwandani hapo kukagua juhudi zinazofanywa na Manispaa ya Ilala.
Ofisa
Mtendaji wa Kata ya Gongo la Mboto Bw. Alphonce Msenduki akikabidhi
taarifa ya kiwanda hicho kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Mazingira Dkt. Terezya Huvisa.
Mgeni
rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya
Huvisa akizungumza na wakazi wa Gongo la Mboto wakati alipotembelea na
kukagua kiwanda cha kuchambua taka (KIKUTA) kilichopo Gongo la Mboto
jijini Dar.
Mh.
Dkt. Huvisa amempongeza Diwani wa Kata hiyo ambaye pia ni Meya wa
Halamshauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa kwa jitihada zake za
kuhamasisha usafi kwenye Manispaa yake na kuzitaka Manispaa zingine
kuiga mfano wa Manispaa ya Ilala ambapo pia amewahamasisha wakazi wa
Gongo la Mboto kutunza Mazingira kwa kupanda miti ili kukabiliana na
manadiliko ya tabianchi yanayopelekea ongezeko la Joto duniani.
Pichani
juu na chini ni Baadhi ya wakazi wa Kata ya Gongo la Mboto
wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt.
Terezya Huvisa (hayupo pichani).
Diwani
wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa
ya Ilala Jerry Silaa akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa wakati wa halfa hiyo. Kulia ni
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Gongo la Mboto Bw. Moshi Mwaluko.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa
(katikati) akielekea kukagua kiwanda hicho akiwa amembatana na Diwani wa
Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya
Ilala Jerry Silaa (kushoto) pamoja na Afisa Usafishaji wa Manispaa ya
Ilala Bw. Samuel Bubegwa (kulia).
Mh.
Dkt. Terezya Huvisa akiangalia maji ya michoro iliyopo katika kiwanda
hicho inayohamasisha suala utunzaji wa Mazingira majumbani.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akipata
maelezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi kiwanda hapo namna
wanavyotengeza Mbolea kwa kutumia taka zilizooza.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akingalia
Mbolea iliyozalishwa kiwanda hapo tayari kwa matumizi.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akikagua
kifaa kinachotumika kuchambulia taka kwa ajili ya kuzalishwa upya
kiwandani hapo.
Mratibu
wa Jamii na miradi kutoka Bremen Overseas Research and Development Bi.
Larissa Duma (kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa (katikati) alipotembelea na
kukagua kiwanda cha KIKUTA. Kushoto ni Diwani wa kata ya Gongo la Mboto
na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
Mgeni
rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya
Huvisa kwenye picha ya pamoja na Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye
pia ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa pamoja wa
wafanyakazi wa kiwanda cha kuchambua taka (KIKUTA).
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akiagana
na Mratibu wa Jamii na miradi kutoka Bremen Overseas Research and
Development Bi. Larissa Duma.
Na.Mwandishi wetu.
Manispaa
ya Ilala katika Kata ya Gongo la Mboto imezindua kiwanda cha kuchambua
taka chenye uwezo wa kutengeneza Mbolea, Mboji na bidhaa mbalimbali
zitokanazo na taka ngumu na nyepesi.
Kiwanda
hicho awa kilijulikana kama kituo cha kutupia taka (KIKUTA) ambacho
kilijengwa na mfadhili Bremen Overseas Research and Development kutoka
Canada.
Kiwanda
hicho cha kipekee kimetokana na juhudi za wakazi wa Gongo la Mboto na
Kikundi cha Gongo la Mboto Youth Group wakisaidiana na viongozi wao na
Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Meya wa Halmashauri ya
Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
Kiwanda hicho kitatoa ajira kwa vijana ili kujikwamua kwenye lindi la umaskini.
CHANZO: MICHUZI MATUKIO
CHANZO: MICHUZI MATUKIO
0 comments:
Post a Comment