Mkurugenzi
wa Masoko na Usambazaji kutoka Wakala wa Mbegu za Kilimo Bw. Philemon
Kawamala akieleza kwa waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam kuhusu
mchango wa wakala huo katika uzalishaji wa mbegu bora za kilimo kwa
kipindi cha misimu sita tangu kuanzishwa. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi
wa Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Masoko na
Usambazaji kutoka Wakala wa Mbeg u za Kilimo Bw. Philemon Kawamala
(hayupo pichani)(Picha na Fatma Salum-Maelezo).
Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) ulianzishwa tarehe 23 Juni, 2006 chini ya sheria ya wakala namba 30 ya mwaka 1997.
Pamoja na majukumu mengine jukukumu kubwa la wakala ni kuongeza uzalishaji na usambazaji wa mbegu bora nchini.
Msimu wa
kwanza wa 2006/2007 wakala ulizalisha tani za mazao mbali mbali 429
ambapo ilikuwa ni sawa na asilimia 2.6 ya soko la mbegu nchini na hadi
kufikia 2011/2012 uzalishaji umeongezeka na kufikia tani 5,542 sawa na
asilimia 19.79 ya soko la mbegu nchini.
Aina Mpya ya Mpunga kwa Afrika (NERICA-series)
Kamati ya
mbegu ya taifa imepitisha aina tano za mpunga wa nchi kavu aina ya AMMKA
au NERICA. Kirefu cha AMMKA ni Aina mpya ya mpunga kwa Africa au kwa
kiingereza NERICA”New Rice for Africa”
AMMKA ni jina linalounganisha aina nyingi za mpunga kwenye kundi moja.
Aina hizi ni NERICA -1, NERICA-2, NERICA-4, NERICA-5 na WAB450.
Kutokana na
hali ya mabadiriko ya tabia nchi na hasa ukame, aina hizi zinavumulia
sana ukame na zinapandwa kwenye maeneo yanayotegemea mvua kama mahindi.
Aina hii
itachangia sana katika kuongeza uzalishaji wa mpunga hapa nchini kwani
maeneo kama haya ni mengi ikilinganishwa na mabonde ya umwagiliaji au
mabonde yanayotegemea mvua.
Natumia fursa hii kuwaambia wakulima wa Tanzania kulima aina hizi mpya za mpunga.
Kwa
wakulima wanaopata mvua za muda mrefu wana nafasi ya kupanda na kuvuna
mara mbili kwa mwaka kwani zinakomaa kwa muda mfupi kwa kutumia siku 90
hadi siku 100 shambani.
Mfumo mpya wa kuhamasisha matumizi ya mbegu bora kwa wakulima kutumia mnyororo wa thamani “ASA-APPROACH”
Mnyororo wa
thamani wa zao husika huanzia upatikanaji wa pembejeo, uzalishaji,
kuvuna, kuongeza thamani na kuuza kwenye masoko yaliyokusudiwa.
Mfumo wa
zamani katika kuandaa teknolojia hadi kuifikisha kwa walengwa haukuwa
ukiangalia sana mahitaji ya soko. Katika mfumo huu wa ASA wakulima na
wasindikaji wanapewa aina 13 za mbegu ya mpunga na kuzitathimini kuanzia
upandaji, utunzaji wa shamba, uvunaji na usindikaji na mwisho wakulima
kwa kushirikiana na wafanya biashara huchagua mbegu ambayo wanajua
itatoa ushindani kwenye soko na mbegu hiyo huzalishwa kwa wingi ili
kukidhi mahitaji yao.
Mfumo huu
tulianza kuujaribu kwenye zao la mpunga na kuongeza matumizi ya mbegu
kutoka tani 60 mwaka 2007 na kufikia tani 1500 mwaka 2012. Katika msimu
wa 2012/13 ASA imefanyakazi na vijiji 120 katika kanda ya kati kwenye
zao la alizeti ambapo tayari mwitikio kwenye matumizi ya mbegu ya
alizeti unaaza kuwa mzuri ikilinganishwa na hapo awali.
0 comments:
Post a Comment