SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, June 6, 2013

Mr Nice apoteza mkataba wake na GrandPa Records

Picture
(picha: The-Star.co.ke)

Mwanamuziki aliyevumbua staili ya muziki ya TAKEU (Tanzania Kenya Uganda), Mtanzania Lukas Mkenda aka Mr Nice amepoteza mkataba wake na kampuni ya kurekodi muziki ya nchini Kenya, kwa kile kilichoelezwa na kampuni hiyo kuwa ni tabia ya Mr Nice ya uvivu, ulevi, asiyeaminika na asiye na ushirikiano.

Zaidi ya maandishi yaliyoandikwa na GrandPa Records kwenye ukurasa wao wa Facebook, pia wamezungumzia suala hilo walipohojiwa na kituo cha EA Radio ambapo wamesema Mr Nice amesema ataendelea kubaki mjini Nairobi nchini Kenya akitafuta kujiweka sawa.

Bofya kifute cha pleya iliyopachikwa hapo chini kusikiliza.

00:00
00:00
Mkataba Mr Nice, GrandPa wavunjika - EA Radio

0 comments:

Post a Comment