SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, June 3, 2013

CHUO CHA UALIMU KASULU KINAKABILIWA NA CHANGAMOTO KUBWA YA UFUNDISHAJI WA SOMO LA IT‏

Mkuu wa Chuo cha Ualimu Kasulu Mkoa wa Kigoma Mwl.Joseph Mwangamila,wa pili toka kushoto akikabidhiwa msaada wa Kompyuta Tano zenye thamani ya shilingi Milioni 6  na mshindi wa”Vodacom Mahela”Bw.Valerian Kamugisha ambae ni mwanafunzi wa chuo hicho kwa niaba ya Vodacom Foundation.Wanaoshuhudia kushoto ni Meneja wa Vodacom Foundation Bi.Grace Lyon na Mwenyekiti wa bodi wa Chuo hicho  Askofu Dkt Gerald Mpango watatu toka kushoto. Mkuu wa Chuo cha Ualimu Kasulu Mkoa wa Kigoma Mwl.Joseph Mwangamila pamoja na Mwenyekiti wa bodi wa Chuo hicho  Askofu Dkt Gerald Mpango wakiwa na nyuso za furaha wakiinua moja ya Kompyuta juu kati ya tano zenye thamani ya shilingi Milioni sita,walizopewa msaada na mshindi wa ”Vodacom Mahela”Bw.Valerian Kamugisha(kulia) ambae ni mwanafunzi wa chuo hicho kwa niaba ya Vodacom Foundation.anaeshuhudia kushoto ni Meneja wa Vodacom Foundation Bi.Grace Lyon. Mkuu wa Chuo cha Ualimu Kasulu Mkoa wa Kigoma Mwl.Joseph Mwangamila(kulia)akimkabidhi sehemu ya msaada wa Kompyuta Tano zenye thamani ya shilingi Milioni 6,Mwanafunzi wa chuo hicho,Rehema Romani,baada ya kukabidhiwa na mshindi wa”Vodacom Mahela”Bw.Valerian Kamugisha,wa pili toka kushoto,kwa niaba ya Vodacom Foundation.Anayeshuhudia kushoto ni Meneja wa Vodacom Foundation, Bi.Grace Lyon. >Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Kasulu Mkoa wa Kigoma wakiwa wamebeba sehemu ya Kompyuta tano zenye thamani ya shilingi milioni 6 baada ya kukabidhiwa  na mwanafunzi wa chuo hicho ambae ni mshindi wa”Vodacom Mahela”Bw.Valerian Kamugisha kwa niaba ya Vodacom Foundation.
CHUO cha Ualimu Kasulu mkoani Kigoma kinakabiliwa na chamomoto kubwa ya ufundishaji wa somo la teknalojia ya habari na mawasiliano (IT), kutokana na ukosefu ya komputa
Akizungumza mwishoni mwa wiki chuoni hapa, mkuu wa chuo hicho Joseph Mwangamila alisema chuo hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo upungufu wa komputa za kujifunzia sambamba na darasa kwa ajili ya masomo kwa vitendo
Akipokea msaada wa komputa sita zenye thamani ya shilingi milioni sita zilizotolewa na kampuni ya Vodacom kupitia Vodacom Foundation, mkuu huyo wa chuo alisema kutokana na upungufu wa komputa, ufundishaji wa somo hilo umekuwa mgumu chuoni hapo
Kwa upande wake, mwenyekiti wa bodi ya chuo hicho Askofu Dkt Gerald Mpango aliiomba Vodacom kufadhili ujenzi wa jengo la darasa moja na vifaa kwa ajili ya mafunzo ya sayansi kwa vitendo.
Aidha mkuu wa chuo hicho Mwl Joseph Mwangamila pamoja na kupongeza Vodacom kwa msaada huo alisisitiza Vodacom kuweka kipaumbele katika mipango  yao kukisaidia chuo kuondokana na changamoto hizo ili kuboresha zaidi mazingira ya elimu chuoni hapo.
Mmoja wa wanafunzui wa chou hicho Elisi Kasongo alisema kuwa dunia ya sasa inahitaji ufahamu zaidi wa teknolojia ya habari ilikwenda sambamba na mahitaji kwa wakati huu,
Kupitia Kompyuta ni rahisi mwalimu kupata mada na vitu mbalimbali vya kufundishia wanafunzi jambo ambalo kukosekana kwakompyuta hufanyafunzo la somo hilo chuoni hapa kuwa gumu hivyo tunahitaji msaada zaidi” alisema mwanafunzi huyo. 
Wanafunzi wa chuo hicho  wameishukuru Vodacom  Tanzania kwa msaada walioutoa nakuahidi kutumia kikamilifu kwa manufaa yao na wanafunzi wajao watakaofundishwa.
Kwamujibu wa Meneja wa Vodacom Foundation Bi. Grace Lyon msaada huo unalenga kupunguza changamoto hiyo inayofanya wanachuo kukosa fursa ya pamoja wakati wa somo hilo
Bi.Grace alisema kuwa, iwapo Kompyuta hizo zitatumiwa vyema na kwa usahihi zitapunguza changamoto ya uhaba wa Kompyuta jambo ambalo litaongeza ufanisi katika somo  hilo chuo ni hapo.
Kompyuta hizo tano zilikabidhi wa kwa niaba ya Vodacom Foundation na mshindi wa shindano la ”Vodacom Mahela” kutoka kigoma Bw.Valerian Kamugisha aliyeshinda shilingi milioni miamoja hivi karibuni.
Aidha mshindi huyo ni mwanafunzi chuoni hapo ambapo meneja Vodacom Foundation Bi.Grace alisema kuwa mshindi huyo ndio chanzo cha chuo hicho kupata msaada wa Kompyuta hizo kutokana na kilio cha mwanachuo huyo juu ya uhaba wa Kompyuta chuoni hapowa katia kikabidhi wa zawadi.

0 comments:

Post a Comment