GARI LA ABIRIA AINA YA HIACE IKIWA IMEGONGANA USO KWA USO NA GARI AINA YA LAND CRUISER
HIZI NI BAADHI YA MAITI ZILIZO OKOLEWA PUNDE BAADA YA AJALI KUTOKEA
HIVI NDIVYO DALADALA HII ILIVYO HARIBIKA BAADA YA AJALI HIYO KUTOKEA
DALADALA IKIWA IMEUMIA VIBAYA
HILI NDILO ENEO AMBAPO AJALI HIYO IMETOKEA
WANANCHI MBALIMBALI WAKIWA KATIKA ENEO LA TUKIO KUSHUHUDIA AJALI HIYO
TINGO WA DALADALA AKIWAANASHUSHWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA
TINGO WA DALADA\LA AKIWA ANAPELEKWA KATIKA MSAADA WA HARAKA RUFAA
MMOJA WA ABIRIA AKIKIMBIZWA KATIKA MSAADA WA HARAKA RUFAA
MWILI WA DEREVA WA DALADALA ALIYE FARIKI PAPO HAPO UKIPELEKWA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI RUFAA
Kaimu kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ndugu Barakaeli Masaki akizungumza na waandishi wa habari.
Picha na Habari na JOSEPH MWAISANGO
Picha na Habari na JOSEPH MWAISANGO
Watu sita wamefariki Dunia na wengine Sita kujeruhiwa katika ajali ya Barabarani iliyo tokea Nanenane Darajani eneo la Uyole Mbeya.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mbeya Barakael Masaki amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwataja marehemu hao kuwa ni pamoja na madereva mmoja wa Hiace.
Masaki amesema dereva wa Hiace amefahamika kwa jina la Meshack Hosea aliye kuwa anaendesha Gari nambali T178 AAV aina ya Toyota Hiace inayofanya kazi Sokomatola na Uyole ambapo muda huo ilikuwa ikitokea Sokomatola kuelekea uyole.
Dereva wa Toyota Land Cruiser Abdalah Ndabagi anashikiliwa na Polisi kwa Mahojiano.
Maiti nne hazijatambuliwa hadi sasa wakiwemo wanawake wanne waliokuwa abiria katika Daladala hiyo na miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa jijini Mbeya.
Aidha amesema majeruhi sita wamelazwa katika hospitali ya Rufaa wakiwemo wanaume watano na Mwanamke mmoja . Ambao mpaka sasa majina yao hayatambuliwa kutokana na kujeruhiwaa vibaya.
Chanzo cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni mwendo kasi wa Magari hayo na wito ameutoa kwa Madereva kuwa makini na kufuata sheria za Barabarani ili kuepusha ajali ambazo zingeweza kutokea. Ikizingatiwa hilo ni eneo la Jiji.
Picha na Mbeya yetu Blog
)
0 comments:
Post a Comment