Miss Earth Tanzania 2012, Bahati Chando (katikati) akizungumza mbele ya wanahabari (hawapo pichani) mapema leo kwenye hoteli ya Lamada, Ilala jijini Dar kuhusiana na uzinduzi wa sherehe yao ya "Mother's Day", siku ya Mama Duniani itakayofanyika Mei 12, 2013 kwenye hoteli hiyo, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu imepangwa kuwa ni "Always in our heart's", "tukiwakumbusha akina mama zetu kwamba wapo moyoni mwetu na tunawapenda sana" alisema Chando. Kushoto ni diwani wa kata ya Kipawa, Mh. Bonnah Kaluwa na kulia ni Mratibu wa hafla hiyo, Bi. Regina Ogwalla. Bahati amesema kuwa katika hafla hiyo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Mwenyekiti wa UWT Ilala, Mh. Nora Mzeru.
Diwani wa Kata ya Kipawa, Mh. Bonnah Kaluwa (kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusiana
na uzinduzi wa sherehe yao ya "Mother's Day" siku ya Mama Duniani itakayofanyika Mei 12, 2013 kwenye hoteli hiyo, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu kwenye hafla hiyo imepangwa kuwa ni "Always in our heart's".
Miss Earth Tanzania 2012,Bahati Chando amesema kuwa ameamua kuungana na Diwani wa kata ya Kipawa,Mh.Bonnah Kaluwa kuandaa hafla hiyo itakayozinduliwa na Wamama wa Ilala,kutambua umuhimu wa kina mama,kuwafurahisha lakini pia kuwaelimisha kuhusu mambo mbalimbali,amesema kuwa amekuwa na shauku kubwa ya kuandaa sherehe kama hiyo ili kujitoa na kusaidia watu kama watu wengi walivyoungana kumsaidia katika safari yake ya kuwa mrembo wa kupeperusha bendera ya Tanzania Kimataifa. Pia anasema kuwa ameandaa sherehe hiyo kuonyesha jamii kwamba,kuwa mrembo au miss sio tu kupozi mbele ya Kamera,bali inaambatana na na jukumu la kugusa jamii kwa namna mbalimbali.

0 comments:
Post a Comment