SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, May 8, 2013

FUNDI UASHI AIBUKA MSHINDI WA MAMILIONI YA AIRTEL‏

Mshindi wa shilingi milioni 15 wa promosheni ya Amka Milionea, Juma Ibrahim Hamza, ambaye ni  fundi uashi akilia kwa furaha na kushindwa kuongea mara baada ya kutangazwa mshindi wa shilingi milioni 15 kupitia promosheni ya Amka Millionea. Airtel imewazawadia washindi wawili wa milioni 15 walioibuka washindi mwezi Machi.
Meneja Uhusiano wa Airtel, Bwana Jackson Mmbando (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi wa shilingi milioni 15 bwana Adnan Ayub Khan mara baada ya kuibuka mshindi wa mwezi wa promosheni ya Amka Millionea. Akishuhudia ni Afisa Masoko wa Airtel, Bi Khalila Mbowe.
Afisa Masoko wa Airtel, Bi Khalila Mbowe (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi wa shilingi milioni 15 bwana Juma Ibrahim Hamza  mara baada ya kuibuka mshindi wa mwezi wa promosheni ya Amka Millionea. Akishuhudia ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Bwana Jackson Mmbando.
Press Release
FUNDI UASHI AIBUKA MSHINDI WA MAMILIONI YA AIRTEL‏
-Washindi wa  Airtel Amka millionea wakabidhiwa shilingi milioni 15
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea kuwazawadia wateja wake kupitia promosheni ya Amka Millione na Airtel ambapo wateja wawili washindi wa mwezi Machi wamezawadiwa kila moja kitita cha shilingi milioni 15 kila mmoja.Washindi hao ni pamoja na bwana Juma Ibrahim Hamza  mwenye umri wa miaka 30 ambaye ni mkazi wa Kawe jijini Dar es Salaam na bwana Adnan Ayub Khan umri wa miaka 25 mfanyabiashara katika mkoa wa Simiyu walijishindia kila mmoja milioni 15.Akiongea wakati wa kukabidhi mfano wa hundi kwa washindi hao, Meneja Uhusiano wa Airtel, bwana Jackson Mmbando alisema, leo tunao washindi wawili waliojishindia shilingi milioni 15 kila moja katika droo ya mwisho wa mwezi Machi. Tumeendelea kushuhudia Watanzania na wateja wetu wakiibuka mamilionea kila siku, kila wiki na kila mwezi kupitia promosheni hii ya Amka Milionea.
Tunaahidi kuendelea kuwazawadia wateja wetu huku tukiboresha huduma zetu, na kuwapata huduma bora zenye gharama nafuu kupitia huduma yetu poa ya Airtel Yatosha inayomuwezesha mteja kuwasiliana na mitandao mingine ya simu za mkononi kwa bei poa na kupata vifurushi vya ujumbe mfupi na huduma ya internet bila kulipia gharama ya ziada. Aliongeza Mmbando
Akizungumza wakati wa makabidhiano, bwana Juma Ibrahim Hamza,  mshindi wa milioni 15 alisema, nashindwa jinsi ya kuongea lakini nashukuru sana Airtel kwa kuweza kunizawadia shilingi milioni 15 ambazo kwangu  ni kama ndoto.  Nategemea kutumia pesa hizi kujenga nyumba yangu ya kuishi pamoja na familia yangu.
Kwa sasa ninajishughulisha na shughuli za ufundi wa kujenga tiles katika nyumba za watu na ninajipatia kipato kidogo ambacho nilijibana na kutumia kiasi kutuma sms wakati wa promosheni ya Amka Milionea ya Airtel. Kama kujaribu bahati yangu na leo nashangaa kuibuka mshindi wa mamilioni haya 15, namshukuru sana Mungu kwa kweli! Alisema bwana Ibrahim
Binafsi nachukua fulsa hii kuwaasa Watanzania kushiriki katika promosheni hizi za Airtel na kwa hakika wataamka washindi kama mimi hivi leoKwa upande wake bwana Adnan Khan ambaye pia ni mshindi alisema, anawashukuru Airtel kwa kuanzisha promosheni ya Amka Millionea, na kuahidi kuzitumia pesa zake kuendeleza na kupanua biashara kwa kuwa hiyo ndio shughuli kubwa anayoifanya.
Promosheni ya Amka Milionea imefika mwisho wake ambapo mpaka sasa wateja zaidi ya1458 na pesa taslimu zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 626 zimezawadiwa kwa washindi walioibuka kutoka katika mikoa mbalimbali nchini.

0 comments:

Post a Comment