Afisa Habari wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro ltd Vidah Fammie.
Baadhi ya Dust bin zinazomilikiwa na
kampuni ya Green Waste Pro ltd. zilizowekwa katika baadhi ya mitaa ya
Manispaa ya Ilala ambazo pia mteja yoyote anapohitaji huuzwa.
--
Na.Mwandishi wetu.
Wananchi wa jiji la Dar es Salaam
hususan wakazi wa manispaa ya Ilala wametakiwa kutambua kuwa suala la
usafi na kutunza mazingira ni jukumu la watu wote na sio tu la kampuni
zilizopewa kandarasi ya kukusanya taka.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Afisa
Habari wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro ltd iliyopewa dhamana ya
kufanya usafi katika manispaa ya Ilala Vidah Fammie amesema katika
kutekeleza majukumu yao ya kila siku wanakabiliana na changamoto nyingi
zikiwemo watu kutochangia katika ulipaji wa ada ya taka na pia kutolipa
kwa muda muafaka.
Akiendelea kuzitaja changamoto hizo
amesema pia wangependa wananchi watambua kuwa suala la dust bin, watu
wamekuwa wakielewa vibaya kuwa wao ndio wanaopaswa kuzimbaza jambo
ambalo sio kweli, kampuni ya usafi ya Green Waste Pro wanaziuza na
hawamlazimishi mteja wao yeyote kununua, ila anaruhusiwa kununua pale
anapopenda, na kuwa zile dust bin zinazowekwa mitaani wao wanapata
usaidizi kutoka manispaa.
Pia ameshauri kwa wale ambao hawana dust
bin watumie mifuko maalum ya kuweka taka na gari litakapopita
litachukuwa kama ulivyo utaratibu wa suala la usafi.
Bi. Vidah Fammie ameongeza kuwa tatizo jingine wanalokabiliana nalo ni suala la upeo mdogo wa wananchi kuhusu suala la usafi.
Mwandishi wa habari hizi alipotaka
ufafanuzi kuhusu suala hilo, amesema inaonekana wapo wananchi wanaoelewa
suala zima la usafi lakini wanapuuzia na kuna wale wasio elewa kabisa
hivyo mtu akiwa na taka anatupa tu kwa kuwa anajua kuna mkandarasi wa
kufanya usafi kitu ambacho si sawa.
Kingine amesema ni miundo mbinu mibovu
na hali ya hewa hivyo wakati mwingine kwa mfano gari maalum la kusafisha
barabara linashindwa kufika hivyo inabidi kutumika nguvu za ziada kama
vile vibajaji na vitu vingine.
CREDIT TO H@KI NGOWI
CREDIT TO H@KI NGOWI
0 comments:
Post a Comment