SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, April 9, 2013

Rais Jakaya Kikwete akutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Millenium Challenge Corporation MCC ikulu jijini Dar leo,Pia apongeza walioshiriki Zoeazi la Uokozi Ajali ya Jengo la Ghorofa Jijini Dar es Salaam

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na kijana mlemavu Shabani Selemani Mohamed katika ukumbi Sabasaba katuka viwanja vya maonesho ya Sabasaba barabara ya Kilwa ,wakati wa hafla fupi ya kupongeza makundi mbalimbali yaliyoshiri katika kazi ya kuokoa watu na kuopoa miili wakati wa ajali ya kuanguka kwa ghorofa katikati ya Jiji la Dar e Salaam hivi karibuni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akioongea na makundi mbalimbali pamoja na vikosi vya ulinzi na usalama vilivyoshiriki katika zoezi la uokozi wakati wa ajali ambapo jengo la ghorofa liliporomoka , kuuwa na kujeruhi watu kadhaa katikati ya Jiji la Dar es Salaam hivi karibun.Hafla hiyo fupi ilifanyika katika ukumbi wa Sabasaba katik viwanja vya maonyesho ya kimataifa ya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam jana
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti cha pongezi kwa Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova kwa uendeshaji wa Zoezi la uokoaji katika ajali ya Jengo lililoporomoka jijini Dar es Salaam hivi karibuni.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick.
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapongeza baadhi ya askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ walishiriki katika kazi ya kuokoa watu wakati wa ajali ya kupomoka kwa jengo katikati ya jiji la Dar es Salaam hivi karibuni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Millenium Challenge Corporation MCC Bwana Daniel Yohannes ikulu jijini Dar es Salaam  jana.Kushoto ni Balozi wa Marekani Alfonso Lenhardt.
Picha na Freddy Maro-IKULU

0 comments:

Post a Comment