SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, March 18, 2013

TAARIFA MAALUM KUTOKA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA:Mwisho wa kuwasilisha maombi Ujumbe wa Mabaraza ya Katiba Jumatano,Machi 20, 2013

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba na Katibu wa Tume Bw. Assaa Rashid.
****

 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIATUME YA MABADILIKO YA KATIBA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mwisho wa kuwasilisha maombi Ujumbe wa Mabaraza ya Katiba Jumatano, Machi 20, 2013 
Tumya Mabadilikya Katiba inapenda kuwakumbushwananchi wotwanaopendkuwWajumbwaMabaraza ya Katiba ya Wilaya kuwa siku ya mwisho ya kuwasilisha maombi hayo kwa Maofisa Watendaji waMitaa na Wilaya kwa Tanzania Bara na Masheha kwa Zanzibar ni siku ya Jumatano, tarehe 20 Machi mwakahuu (2013).Wananchi wanaopendkuwWajumbwa Mabaraza haywawasilishe maombi yao yakiwa na taarifazifuatazo: Majina Kamili; Jinsi; Umri; Eneo analoishi kwenye Kijiji/Mtaa; Kiwango cha Elimu; na Kazi yake.Mwombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo: Awe ni Raia wa Tanzania na awe na umri wa miaka 18 au zaidi naawe na uwezo wa kusoma na kuandika. Sifa nyingine ni pamoja na kuwa mkazi wa kudumu wa kijiji, mtaa aushehia husika na awe ni mtu mwenye hekima, busara na uadilifu na pia awe mtu mwenye uwezo wa kujielezana kupambanua mambo.
Kuhusu ukazi wa kudumu
Kuhusu ukazi wa kudumu, Tume inapenda kuwafahamisha wananchi kuwa mkazi wa kudumu ni mwananchiyeyote anayeishi katika mtaa au kijiji husika na sio lazima awe anamiliki nyumba katika mtaa au kijiji hicho. Aidha, Tume inapenda kuwafahamiusha wananchi walioomba kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilayakuhakiki majina katika orodha ya majina ya waombaji wote itakayobandikwa katika eneo la wazi au mbao zamatangazo katika Mtaa, Kijiji au Shehia husika kwa siku saba kuanzia tarehe 22 hadi tarehe 28 mwezi machimwaka huu (2013).
Tarehe za uchaguzi wa Wajumbe ngazi ya Mtaa na Kijiji
 Aidha, Tume inapenda kuwafahamisha wananchi kuwa imefanya mabadiliko madogo katika mwongozo wakekatika tarehe za vikao vya mitaa na vijiji vitakavyowachagua Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba. Kwa mujibu wamwongozo uliotolewa na Tume mwezi uliopita, vikao hivi vilipaswa kufanyika kati ya tarehe 30 mwezi Machimwaka huu (2013) na tarehe 3 Aprili mwaka huu (2013).Kwa mujibu wa mabadiliko mapya, vikao hivyo sasa vitafanyika kati ya tarehe 30 Machi mwaka huu (2013) haditarehe 5 Aprili mwaka huu (2013). Kwa msingi huu kila kijiji au mtaa kitachagua tarehe atika vikao hivyo,wananchi watapiga kura za siri kuwachagua wananchi wanne kuwa Wajumbe wa Mabaraza ya Katiba yaWilaya.Kufuatia mabadiliko haya, Vikao Maalum vya Kamati za Maendeleo za Kata vya kuwachagua wajumbe wannekutoka miongoni mwa wananchwaliochaguliwna vijiji na mitaa navyo vimesogezwa mbele na sasavitafanyika kati ya tarehe 7 Aprili mwaka huu (2013) na tarehe 10 Aprili mwaka huu (2013). Awali, vikao hivivilipangwa kufanyika kati ya tarehe 5 Aprili mwaka huu (2013) na tarehe 9 Aprili mwaka huu (2013).Tume inawaomba wananchi kushiriki na kuendesha mchakato wa kuwapata Wajumbe kwa amani na utulivu nakuzingatia mwongozo uliotolewa na Tume.
Imetolewa na:
Tume ya Mabadiliko ya Katiba,Dar es Salaam
Machi 18, 2013
 

0 comments:

Post a Comment