VIONGOZI mbalimbali wa kitaifa wameendelea kufika katika
Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam ili kumjulia hali Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba, ambaye amelazwa
katika chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU).
Mke wa Waziri Mkuu, Tunu Pinda, Ofisa Mwandamizi
Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Jamal Rwambow ni miongoni mwa viongozi ambao
walifika hospitalini hapo jana na kupata fursa ya kumwona Manumba,
wakati juzi Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilali naye alimtembelea.
Viongozi wengine ambao wamemtembelea Manumba ni pamoja na Rais Jakaya Kikwete na mke wake, Mama Salma Kikwete.
Wengine ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk
Emmanuel Nchimbi, Naibu wake Pereira Silima, Msajili wa Vyama vya Siasa
nchini, John Tendwa, Mkuu waJeshi la Polisi nchini, Said Mwema pamoja na
maofisa wengine wa vyeo vya juu wa jeshi hilo.
Taarifa iliyotolewa jana na uongozi wa Hospitali ya Aga Khan, imeeleza kuwa DCI Manumba bado anaendelea kutibiwa akiwa chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari na wauguzi.
Taarifa iliyotolewa jana na uongozi wa Hospitali ya Aga Khan, imeeleza kuwa DCI Manumba bado anaendelea kutibiwa akiwa chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari na wauguzi.
“Uongozi wa Hospitali ya Aga Khan unapenda
kuujulisha umma kwamba Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai
nchini, (DCI) Robert Manumba bado yupo hospitalini, ambapo anaendelea
kupatiwa matibabu.
“Hali ya afya yake bado inahitaji uangalizi wa karibu wa madaktari na wauguzi,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk Jaffer Dharsee
alisema kwamba kesho atazungumzia kwa kina kuhusu matatizo yanayomsumbua
Manumba hasa baada ya majibu ya vipimo alivyofanyiwa juzi na jana.Kwa habari zaidi bofya na Endelea........>>>>
0 comments:
Post a Comment