Mimi nadhani umefika wakati sasa Jeshi la Polisi likisaidiwa na Raia wema na hata JWTZ wafanye ukaguzi wa silaha nchi nzima. Kuna silaha zimezagaa sana nchini sasa tunashidwa kuelewa kwa nini Serekali inakaa kimya na Watanzania wema wanazidi kupata matatizo. Hili si swala la kujadili tena kwani matukio ya watu kupigwa risasi yamezidi sana. Polisi wenyewe mmejionea. Zamani watu walikuwa waoga sana kupiga Polisi sasa hivi tokea Polisi nao kutembeza mkong’oto kwa raia bila mpangilio wamejikuta wakipata adha ya kupata kipigo na pingine kupigwa risasi.
Mikoa na majiji yaliyozidi sana ambayo inabidi Silaha zote zisalimishwe Polisi kwa ukaguzi upya ni Dar es salaam, Mbeya, Mwanza, Arusha, Moshi, Musoma, Morogorio, Kigoma, Tabora, Dodoma, Tanga, Manyara, Bukoba nk. Tunaomba Jeshi la Polisi kufanya utaratibu wa kukagua silaha hizo nchi nzima tena kwa wakati mmoja ili kujipunguzia majukumu ya kupambana na uhalifu. Endapo watu watasajili silaha zao upya italeta unafuu wa kuwajua watu wenye silaha halali na wenye silaha haramu. Tusipofanye hivyo raia wema wataendelea kuishi kwa mashaka na hata nyie Polisi mtajikuta mnafanya kazi kwa matatizo sana.
Trafic Polisi wapewe silaha hasa katika vizuizi muhimu kama wafanyavyo wenzetu kule Kenya na Uganda. Unakuta Polisi wako kwenye vizuizi vya barabara kubwa lakini mikono mitupu. Huu ni ulimwengu wa shari silaha mnawacha ofisini ili zifanye kazi gani muhimu. Hakikisheni kila kizuizi kinakuwa na hata bunduki 2 zenye risasi za kutosha. Tusifanye mzaha na usalama wa raia kwani tumekaribisha watu wa aina nyingi sana nchini wengine kihalali na wengine hata hatuwajui. Hii ndiyo hasara ya kukaribisha watu wa nje. Wengine wanakuja kwa uzuri wengine kwa ubaya. Ili kupunguza wimbi la watu kuja nchini kufanya kazi pandisheni bei za vibali vya kufanya kazi. Binadamu ukimzuia kwa maneno anakuwa mkorofi muwekee sheria kali na zitekelezeke.
Unampa mgeni umeneja wa Hotel au Kampuni lakini haujui historia yake. Unampa mgeni kazi ya upishi wa Hoteli hata haujui Historia yake. Tanzania tumekimbilia mambo mengine bila hata kujua faida na hasara zake. Mwisho na nyie Polisi utendaji wenu uko chini ya viwango kwa ajili ya kupenda rushwa. Mnakimbilia kuchukua rushwa bila kufanya ukaguzi wa magari yanayoingia na kutoka nchini. Pembe za Tembo zinapotaje mpaka Airport au bandarini kama sio mnakimbilia rushwa. Twiga anapakiwaje kwenye ndege kama sio mnakimbilia rushwa. Fanyeni kazi bwana mnatia nchi kwenye umasikini na uhalifu usio na sababu.
Mkereketwa
Gilliard David
|
Sunday, November 4, 2012
SILAHA ZIKAGULIWE UPYA.
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Sunday, November 04, 2012
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Labels:
SILAHA ZIKAGULIWE UPYA.
0 comments:
Post a Comment