SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, October 2, 2012

BILIONI 280 KUSAIDIA USAMBAZAJI WA MAJI KATIKA JIJI LA DAR NA CHALINZE.


Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa(kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waaandishi wa habari jana jijini Dar es salaam mara baada ya india kupitia Benki ya Exim kuikopesha Tanzania shilingi bilioni 280 kwa ajili kusaidia kusambza maji katika Jiji la dare s salaam na mji wa Chalinze.  Kulia ni Meneja Mkuu wa Benki ya Exim ya India Geeta Poojary.

Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa(kushoto) akibadilishana hati ya mkopo wa shilingi bilioni 280 kutoka kwa  Meneja Mkuu wa Benki ya Exim ya India Geeta Poojary(katikati) jana jijini Dar es salaam kwa ajili ya kusaidia usambzaji wa maji mji wa Chalinze na Jiji la Dar es salaam. Kulia ni Balozi wa India Debnath Shaw.(Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam).
==**==
Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam



Serikali ya India kupitia Benki ya EXIM imeikopesha Tanzania shilingi bilioni 280 kwa ajili ya usambazaji maji katika Jiji la Dar es salaam na mji wa Chalinze mkoani Pwani.

Mkopo huo umesainiwa jijini Dar es salaam na Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa kwa upande wa Tanzania  na Meneja Mkuu wa Benki ya EXIM ya india Bibi Geeta Poojary.

Akizungumza mara baada ya kusaini mkopo huo Waziri wa Fedha alisema kuwa mkopo huo umekuja kwa wakati ili kuisaidia Tanzania kukabilina na uhaba wa maji katika jiji la Dar es salaam na maeneo ya Chalinze mkoani Pwani.

Alisema kuwa hatua hiyo itasaidia kuboresha huduma za jamiii na kiuchumi kwa wakazi wa maeneo husika badala ya kutumia muda mwingi kutafuta maji badala yake wautumie katika kujiongezea kipato na kukabiliana na umasikini.

Dr. Mgimwa alisema kuwa mradi huo utasaidia kuongeza uzalishaji wa maji kutoka mita za ujazo milioni 82 hadi kufikia mita za ujazo milioni 196 kwa siku.

Aliongeza kuwa pia mradi huo utahusisha ujenzi wa njia ya usafirishaji wa maji na kuongeza mtandao wa usambazaji kwa wateja.

Dr. Mgimwa aliongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo itakuwa sehemu ya kutekeleza Mkakati wa Kukuza Uchumi na kupunguza Umaskini(MKUKUTA) na kupunguza magonjwa yatokana na maji yasiyokuwa salama.

Alisema kuwa Tanzania itatakiwa kulipa  mkopo huo kwa kipindi cha miaka ishirini (20) ambapo kabla ya kuanza kulipa Tanzania itakuwa  miaka mitano ya unafuu (grace period) kabla ya kuanza malipo.

Dr. Mgimwa aliongeza kuwa mkopo huo ni moja ya mikopo nafuu sana kwani Tanzania itatakiwa kulipa riba ya asilimia  1.75 ya mkopo .

0 comments:

Post a Comment