Ofisa
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom
Tanzania Mwamvita Makamba akikabidhi sehemu ya sadaka ya futari kwa
watoto wa madrasa za wilayani Mafia yenye thamani ya zadi ya shilingi
milioni tisa. Vodacom kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom
Foundation ilikabidhi sadaka ya futari kwa watoto zaidi ya mia tatu wa
kisiwani Mafia hafla iliyoambatana pia na kufuturisha katika msikiti
mkuu wa Wilaya mwishoni mwa wiki. Wanaoshudia makabidhiano hayo ni Mkuu
wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule na Imam Mkuu wa Msikiti wa
Wilaya Ally Mwabaku.
Wanafunzi
wa Madrasatul Shamsia ya Mjini Mafia wakipokea kwa furaha katoni ya
sabuni kutoka kwa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa kampuni ya Mawasiliano
ya Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba.Vodacom kupitia mfuko wake wa
kusaidia jamii wa Vodacom Foundation ilitoa pia sadaka ya vyakula kwa
ajili ya futari kwa wanafunzi zaidi ya mia tatu wa madrasa mbalimbali
wilayani humo pamoja na kuwafuturisha mwishoni mwa wiki.Wanaoshuhudia ni
Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule (katikati) na Imam
Mkuu wa Msikiti mkuu wa Wilayani Ally Mwabaku.
Mkuu
wa mfuko wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom wa kusaidia jamii wa
Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule akimhudumia moja ya waumini wa
dini ya Kiislamu wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na mfuko
huo katika msikiti mkuu wa wilaya Qadiriya na kuhudhuriwa na waislamu
mbalimbali wakiwemo watoto zaidi ya mia tatu kutoka madrasa za mjini na
vijijini zilzopo wilayani humo ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Vodacom
share and care ambapo kwa mwezi wa mfungo wa Ramadhani hulenga
kufuturisha waislamu sehemu mbalimbali na kutoa sadaka ya futari kwa
yatima na wajane
Meneja
Mawasiliano wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania Salum Mwalim
akimhudumia futari shekhe Mkuu wa Wilaya ya Mafia Sheikh Yusuf Selemani
wakati wa hafla ya kufuturisha wasilamu na watoto wa madrasa kisiwani
Mafia iliyoandaliwa na Vodacom Foundation ambayo ni sehemu ya kampeni ya
Vodacom ya kila mwaka ya share and care ambapo kwa mwezi wa mfungo wa
Ramadhani hulenga kufuturisha waislamu sehemu mbalimbali na kutoa sadaka
ya futari kwa yatima na wajane.
Wanafunzi
wa Al-Madrasatul Hairislamia ya Mjini Mafia kwa furaha wakibeba kiroba
cha mchele mara baada ya kukabidhiwa msaada wa sadaka ya futari kwa
ajili ya mfungo wa Ramadhani. Vodacom kupitia mfuko wake wa kusaidia
jamii wa Vodacom Foundation ilikabidhi sadaka kwa wanafunzi zaidi ya mia
tatu wa madrasa mbalimbali za kisiwani Mafia yenye thamani ya zadi ya
shilingi milioni tisa ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Share and Care
ambapo kwa mwezi wa Ramadhan hulenga kufuturisha waislamu na kutoa
sadaka ya futari kwa watoto hususan yatima na pia wajane.
Na Haki Ngowi.
0 comments:
Post a Comment