Bao la Nani dakika ya 94 ya mchezo,
liliiwezesha Manchester United kurejea katika mchezo kwa mtindo wa aina yake,
ambapo hadi mapumziko walikuwa nyuma kwa mabao 2-0 na kufanikiwa kuwalaza
mahasimu wao wakubwa wa mji mmoja Manchester City mabao 3-2 na kunyakua Ngao ya
Hisani.
Huku kila mtu akiwa anajua mpambano
huo utachezwa dakika 30 za nyongeza na hata ikibidi mshindi kupatikana kwa
mikwaju ya penalti, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno, aliivuruga ngome
ya Manchester City na kutimua mbio kasi sana na kumzidi mlinzi Kompany baada ya
kusogezewa pande kutoka kwa Wayne Rooney, akamzunguka mlinda mlango wa City Joe
Hart na kuujaza mpira wavuni pasi na wasiwasi. Lilikuwa bao zuri la tatu na la
ushindi kwa Manchester United.
City waliongoza kwa mabao 2-0 hadi
wakati wa mapumziko baada ya mlinda mlango mwanagenzi wa United, Mhispania
David De Gea kuonekana akibabaika na kushindwa kuucheza mpira wa juu wa krosi,
hali iliyomfanya Joleon Lescott kupachika bao kwa kichwa na pia bao la pili la
mkwaju wa mbali uliopigwa na Edin Dzeko.
Lakini United, wakiwa wanajua mechi
zao mbili za mwisho katika uwanja wa Wembley walipoteza, kufungwa na Barcelona
katika fainali ya Ubingwa wa Ulaya, pia kulazwa na Manchester City katika nusu
fainali ya kombe la FA, walibadilika na kujipanga vizuri na kuweza kuwanyima
raha majirani wao na hatimaye wakarejesha mabao mawili haraka haraka.
Chris Smalling alikuwa wa kwanza
kupunguza deni la mabao, baada ya kuunganisha mkwaju wa adhabu ndogo
uliochongwa na Ashley Young kabla Nani kusawazisha kabla ya kuandika bao la
tatu dakika ya mwisho ya mchezo.
Kwa uhaki vijana wa Sir Alex Ferguson
walipoteana wakati Manchester City walipofunga mabao yao ya haraka, huku winga
wao mpya Young akionekana kuzoea mazingira mapya.
Manchester City, kwa upande mwengine
walikuwa wakitumia vyema kila idara uwanjani na walichokusudia katika kipindi
cha kwanza ni kumfanya mwamuzi Phil Dowd awe na kibarua kigumu, huku mlinzi
Micah Richards akiwa miongoni mwa wachezaji wanne waliooneshwa kadi ya manjano
kwa kumchezea vibaya Young.
u wao wakubwa wa mji mmoja Manchester City mabao 3-2 na kunyakua Ngao ya
Hisani.
Manchester United wakishangilia Ngao
ya Hisani

0 comments:
Post a Comment