SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, May 19, 2011

MKUU WA IMF AAMUA KUJIUZULU WADHIFA WAKE!!!

Mkuu wa shirika la fedha duniani Dominique Strauss Kahn ameamua kujiuzulu wadhfa wake katika taarifa iliyochapishwa katika wavuti wa shirika hilo.
Strauss Kahn ametuma taarifa yake kwa bodi ya shirika hilo huku akisema kuwa anakanusha mashtaka yote dhidi yake na amesikitishwa sana na tukio hilo lililomkabili.
Shirika hilo limesema kuwa litatangaza hivi karibuni utaratibu wa kumteua mkurugenzi mpya lakini kwa sasa John Lipsky ataendelea kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa IMF.
Awali Waziri wa Fedha wa Marekani alisema kuwa Mkuu wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Dominique Strauss-Kahn, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya kujaribu kumbaka mhudumu wa hoteli, hawezi tena kuendesha shughuli za shirika hilo.
Timothy Geithner ametoa wito kwa IMF kumteua rasmi Kaimu Mkuu wa Shirika hilo.
Strauss-Kahn anashikiliwa katika jela moja mjini New York baada ya kukamatwa hapo siku ya Jumamosi iliyopita kwa kosa la kujaribu kumbaka mhudumu wa hoteli.
Strauss-Kahn ambaye amezuiliwa katika gereza la wafungwa sugu la Rikers Islands mjini New York, yupo chini ya ulinzi mkali kuchunga asijaribu kujiua.
Wakili wa Mwanamke huyo kutoka Guinea – Afrika Magharibi anayemtuhumu Strauss-Kahn, amesema mteja wake amepata mshutuko ambao sio wa kawaida.
Wakili huyo ameongeza kuwa kwa sasa yupo mafichoni na kwamba anajihisi ”Yuko pekee duniani”.
Strauss-Kahn mwenye umri wa miaka 62, anakabiliwa na mashtaka saba dhidi yake na iwapo atapatikana na hatia, atahukumiwa kifungo cha hadi miaka 25 jela.
Anashtakiwa kwa vitendo vya uhalifu vinavyohusiana na ngono, jaribio la kubaka, udhalilishaji wa kijinsia, kumfungia kinyume cha sheria na kumshika bila ridhaa yake.

0 comments:

Post a Comment