SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Thursday, May 19, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKAGUA UJENZI WA BARABARA YA MIZINGANI PEMBA!!!

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiangalia maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Mizingani Wambaa yenye urefu wa Kilometa 9.7 inayoendelea kujengwa wakati alipotembelea na kukagua akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya Serikali kwenye mikoa ya Kaskazini na Kusini Pemba.  
Kushoto ni Ofisa msimamizi kutoka Wizara yaMaswasiliano na Miundombinu Zanzibar, Hamadi Baucha.  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal akisikiliza maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Mizingani Wambaa yenye urefu wa Kilometa 9.7 kutoka kwa Injinia Gaitano Musuku (kushoto kwake)  wakati alipotembelea na kukagua akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya Serikali kwenye mikoa ya Kaskazini na Kusini Pemba . Kushoto ni Ofisa msimamizi kutoka Wizara ya Maswasiliano na Miundo mbinu Zanzibar, Hamadi Baucha. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal akikagua maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Mizingani Wambaa inayojengwa kwa kiwango cha lami 
yenye urefu wa Kilomita 9.7 wakati alipofika Mkoa wa Kusini Pemba kukagua maendeleo ya miradi ya Serikali. 
(Picha na Muhidin Sufiani-OMR).

0 comments:

Post a Comment