SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Sunday, May 8, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILALA AWASILI UTURUKI KUMWAKILISHA RAIS KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na  Dkt. Mbaraka Lijohiy baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Ataturk, Istanbul jana Mei 7.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiongozana na mkewe Mama Zakhia Bilal na baadhi ya viongozi alioongozana nao baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa ndege wa Ataturk, Istanbul jana Mei 7,kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 4 wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo ya nchi maskini. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Sundery baada ya Dkt. Bilal kuwasili mjini Istambul jana Mei 7, 2011. 
Makamu wa Rais yuko nchini Uturuki kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika mkutano wa Umoja wa Matifa unahusu maendeleo ya nchi maskini, Mkutano huo unaanza leo na kumalizika Mei 13, 2011. Kushoto ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.
 Makamu wa Rais, akiwa katika picha ya pamoja na Dkt. Mbaraka Ljohiy, ambaye ni Mkurugenzi wa Plastic , Reconstructive, Esthetic Had and Microsurgeory (kulia) na mfanyabiashara aishie nchini Uturuki, Ally Kilumba baada ya kukutana nao jana alipowasili jijini Instanbul, kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 4 wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo ya nchi maskini.
Picha kwa hisani ya Ofisi ya Makamu wa Rais).
**********************
ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NCHINI UTURUKI MEI 09-13, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Tanzania Dk Mohamed Gharib Bilal amewasili jana jijini Istambul, Uturuki kuhudhuria mkutano wa nne wa Umoja wa Mataifa, unaohusu maendeleo ya nchi maskini.
Dk Bilal amehudhuria mkutano huu akimwakilisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete na pamoja na mambo mengine atapata fursa ya kuhudhuria mijadala mbalimbali inayohusu nafasi ya maendeleo kwa nchi maskini sambamba na ushiriki wa nchi zenye uwezo wa kiuchumi katika kusaidia harakati za kunyanyua uchumi wa nchi maskini kabisa duniani.
Mkutano huu unalenga kufanya tathmini ya miaka kumi baada ya mkutano wa tatu uliofanyika jijini Brussels mwaka 2001. Makamu wa Rais katika msafara wake ameambatana na Mama Zakhia Bilal sambamba na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, Waziri Kutoka Ofisi ya Rais Zanzibar, Dk Mwinyihaji Makame na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi J. Maalim.
Mkutano huu wa Umoja wa Mataifa kwa nchi maskini, utafanya mijadala itakayohusisha nafasi za serikali, wabunge na Asasi za Kiraia ambazo zote zina uwakilishi kutoka Tanzania.
Imetolewa na: Boniphace Makene.
Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais.

0 comments:

Post a Comment