SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, May 18, 2011

IMF YASHINIKIZWA KUFANYA UTEUZI MPYA!!

Mkuu wa IMF Dominique Strauss
Waziri wa fedha wa Marekani amesema kuwa mkuu wa shirika la fedha duniani (IMF), Dominique Strauss-Kahn, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya kujaribu kumbaka mhudumu wa hoteli, hawezi tena kuendesha shughuli za shirika hilo.
Timothy Geithner ametoa wito kwa IMF kumteua rasmi kaimu mkuu wa shirika hilo.
Bwana Strauss-Kahn anazuiliwa katika jela moja mjini New York baada ya kukamatwa hapo jumamosi kwa kosa la kujaribu kumbaka mhudumu wa hoteli moja.
Strauss-kahn ambaye amezuiliwa katika gereza la wafungwa sugu la Rikers Islands mjini New York yupo chini ya ulinzi mkali kuchunga asijiue. Hii ni baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.
Wakili wa mwanamke huyo kutoka Guinea, Afrika Magharibi, anayemtuhumu Strauss-Kahn, amesema mteja wake amepata mshutuko ambao sio wakawaida.
Wakili huyo ameongeza kuwa kwa sasa yupo mafichoni na kwamba anajihisi ''Yuko pekee duniani''.
Strauss-Kahn, mwenye umri wa miaka 62, anakabiliwa na mashtaka saba dhidi yake na iwapo atapatikana na hatia, atahukumiwa kifungo cha hadi miaka 25 jela.

0 comments:

Post a Comment