SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, December 20, 2010

RAIS ZANZIBAR AAHIDI KUTEKELEZA AHADI ZA WAKATI WA KAMPENI
Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein.
Wanawake wa rika zote visiwani Zanzibar wametakiwa kutokuwa na hofu na kuhakikishiwa kuwa ahadi zote zilizotolewa na rais wakati wa kampeni zinazowahusu wao zitatekelezwa bila ya waiswasi.
Akizungumza katika viwanja vya Kisonge rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein amesisitiza kuwa ahadi zote zitatekelezwa, ikiwemo sera ya wanawake na kundaa mpango maalum ili kuhakikisha wanawake nao wanapata nafasi za juu za kuongoza.
Rais huyo wa Zanzibar pia aliahidi kuwa serikali itahakikisha inapambana na vitendo vilivyoshamiri vya udhalilishaji wanavyofanyiwa wanawake na watoto.
Aidha nao  viongozi wa Umoja wa Wanawake akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja huo Bi. Amina Nassor na Makamu Mwenyekiti Zanzibar Bi. Asha Bakari pamoja na kumpongeza rais huyo pia walitoa wito kwa wanawake visiwani humo kuanza kujiandaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

0 comments:

Post a Comment