SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Monday, December 20, 2010

MSHINDI WA BONGO STAR SEARCH APATIKANA
Mshindi wa shindano la Bongo Star Search 2010 ni Mariam Mohamed(pichani).Hafla ya kumpata mshindi wa shindano hilo ilifanyikia katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar-es-salaam mwishoni mwa wiki.
Jaji Salama Jabir akitoa maoni kwa mshiriki. Salama amekuwa kivutio kikubwa sana katika mashindano hayo kutokana na maoni anayotoa kwa washiriki lakini mashabiki wanamchukulia kama ni mtu mwenye kukatisha tamaa na kujilopekea tu la hasha, hiyo ni fani yake na anajua anachokifanya.
Nimekwambia kaa chini mimi ndio boss wako-Chief Judge Madam Ritha Paulsen akimkaripia kwa kumkalisha Jaji Master J baada ya kuwa mkaidi katika fainali hizo.
Mshiriki Joseph Pyne ambaye alishika nafasi ya 3 katika fainali hizo aliteka ukumbi mzima kwa kushangiliwa na kutunzwa pesa nyingi jukwaani kila alipopanda na kufanya mashabiki wake kuacha midomo wazi kutokana na kuimbia nyimbo ambazo mashabiki wanazikubali na kuzipenda.
Pichani ni baadhi ya mashabiki wa Joseph Pyne wakihamaki kwa kutoamini alichokuwa akiimba mshiriki huyo. Hebu tazama picha hii kwa umakini kila shabiki anaonekana kuhamaki wenggine waliamua kusimama wakiona kwamba wakika chini hawatofaidi vizuri..!!!
Wewe kuchukua milioni 30 usiku wa leo! i will shoot my self- Salama. Hayo ni maoni ya Jaji Salama Jabir kwa Mshiriki Joseph Pyne kwa mtazamo wake kwamba asipate kichwa kuona ukumbi nzima ukipiga nderemo kwa ajili yake.
Vijana wa THT wakitoa burudani wakati wa mapumziko mafupi huku washiriki wa BSS 2010 wakisubiri kufanyiwa mchujo wa raundi ya pili katika fainali hizo.
Mwanamuziki Mwasiti Almasi akitoa burudani katika fainali hizo.
TOP 5 ya BSS 2010 wakisubiri kuchujwa kuingia raundi ya pili katika fainali hizo ambapo mshiriki Waiziri Salum (wa kwanza kulia) alienguliwa na kuaga mashindano hayo lakini hakuondoka mikono mitupu alipata kitita cha shilingi milioni 1 kutoka Bench Mark Production pamoja na Ofa ya kurekodi nyimbo moja katika studio za MJ RECORDS pamoja na cheti cha kushiriki mashindano hayo.
Mother House wa jumba la BSS 2010 naye alikuwepo akishuhudia watoto wake walibyokuwa wakitawala jukwaa katika fainali hizo.
Msanii Cindy kutoka Uganda akikogonga nyoyo za mashabiki wake  katika ukumbi wa Mlimani City.
Beatrice Singano kutoka Airtel ambao walidhamini zawadi ya washindi mshindi wa 2 na 3 katika fainali za BSS 2010 akijiandaa kutangaza washindi walioshika nafasi hizo ambapo bahasha zenye majina ya washindi zikiwa mikononi mwa Mkurugenzi wa Bench Mark Production Madam Ritha Paulsen
Beatrice Singano, akimkabidhi Hundi ya Sh. milioni 10, kwa mshindi wa pili wa fainali za shindano hilo, James Martin anayeshuhudia tukio hilo ni Chief Judge Madam Ritha Paulsen. Washiriki wote walikabidhiwa na vyeti vy kushiriki vilivyotolewa na Kampuni ya Bench Mark.
Beatrice Singano akikabidhi hundi ya Shilingi milioni 5 kwa Mshindi wa tatu  Joseph Pyne.
Mariam Mohamed akionyesha furaha isiyo na kifani baada ya kutangazwa mshindi wa kwanza.
eeeh Mungu..!!! asante kwa kusikia kilio changu na kutimiza ndoto zangu-Mariam Mohamed.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, akimkabidhi Hundi ya Sh. milioni 30, mshindi wa fainali za shindano la Bongo Star Search, Mariam Mohammed, baada ya kutangazwa mshindi. Katikati ni Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark Production, Ritha Paulsen. Mbali na hundi hiyo Mariam alipata zawadi ya Bima ya afya kutoka AAR yenye thamani ya dola 150,000, Pesa taslim shilingi milioni 1 kutoka Mariedo Boutique na zawadi nyingine kibao.
Mariam baada ya kupokea hundi yake aliona asiondoke hivi hivi na kuwapa raha mashabiki wake waliompa ushindi huo na kuanza kucheza.

0 comments:

Post a Comment