Arsenal yampoteza tena Fabregas
Matumaini ya Arsenal kusonga mbele hatua ya timu 16 ya kuwania Ubingwa wa soka wa Ulaya, yalizidi kuingia mashakani baada yakufungwa na Braga mabao 2-0 na vile vile wachezaji wake wakutumainiwa, nahodha Cesc Fabregas na Emmanuel Eboue kuumia.
Cesc Fabrega
The Gunners baada ya kupoteza mchezo huo, hivi sasa hawana budi kujifunga kibwebwe na kushinda mchezo wao wa mwisho wa hatua ya kufuzu ili kujihakikishia kusonga mbele.
Nahodha Fabregas aliumia misuli ya paja, wakati Eboue ameumia goti.
Kwa mujibu wa meneja wa Arsenal, Arsene Wenger: "Huenda ikamchukua wiki mbili au tatu Fabregas kupona. Aliongeza "Nilibahatisha kumchezesha na sasa mambo yameharibika."
Wenger alimchagua Fabregas kucheza licha ya kiungo huyo kutokuwa katika hali yake ya kawaida. Amesema, ni tatizo la msuli wa paja katika mguu mwengine, ni vigumu sana kutabiri kwa muda gani Cesc hatacheza.
Alipoulizwa iwapo hatacheza mchezo wa Jumamosi wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Aston Villa, Wenger alijibu: "Hakika hataweza."
Akaongeza: "Eboue hataweza kucheza kwa wiki chache zijazo kwa sababu alifanyiwa rafu mbaya, ambayo mwamuzi hakutoa adhabu."
Wenger, ambaye alishuhudia Carlos Vela akikataliwa kupewa adhabu ya mkwaju wa penalti, wakati timu hizo zilipokuwa sare ya 0-0, hakufurahishwa na waamuzi kuhusiana na kuumizwa kwa Ebue na kuongeza: "Ni kazi gani mwamuzi wa tano anafanya? Tunaelekea kipindi kigumu tusichokuwa na bahati nacho."
Arsenal ilikuwa inahitaji pointi kuweza kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele hatua ya mtoano, lakini wakazembea na kuruhusu mabao mawili yaliyofungwa na Matheus dakika ya 83 na jingine kutoka kwa Mbrazil huyo katika dakika za nyongeza kwenye uwanja wa Estadio Municipal.
0 comments:
Post a Comment