Kikwete atangaza Baraza jipya la mawaziri Tanzania
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania ametangaza baraza jipya la mawaziri huku mawaziri wengi waandamizi wakiendelea kushikilia nafasi walizokuwa nazo katika serikali iliyopita. Kikwete ametangaza baraza jipya la mawaziri baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 31 uliogubikwa na madai ya wizi wa kura na idadi ndogo ya wapiga kura. Akizungmza na waandishi habari, Kikwete amesema kuwa baada ya kutathmini muundo wa serikali, ameridhishwa na utendaji wa baraza la mawaziri alililoteua mwaka 2008 na hivyo hakufanya mabadiliko makubwa. Mawaziri waandamizi waliosalia katika nafasi zao ni Mustafa Mkulo wa Fedha na Masuala ya Uchumi na Bernard Membe wa Mambo ya Kigeni na Ushirikiano wa Kimataifa. Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja amebakia katika nafasi yake sawa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Hussein Mwinyi. Kati ya nyuso mpya katika baraza la mawaziri Tanzania ni Anna Tibaijuka mkurugenzi wa zamani wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi UN HABITAT ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kikwete pia ambuni wizara mpya itakayoshughulikia uwekezaji wa kigeni. Kwa ujumla rais Kikwete ameteua Baraza la mawaziri lenye idadi ya nafasi 50 wakiwemo manaibu mawaziri na nyuso 24 mpya. Baraza lililipota la mawaziri lilikuwa na nafasi 47.
Baraza jipya la mawaziri Tanzania linatazamiwa kuapishwa siku ya Jumamosi katika viwanja vya Ikulu ya Dar Es Salaam.
Orodha kamili ya mawaziri na manaibu waziri ni kama ifuatavyo:
1. Ofisi ya Rais (Utawala Bora): Mathias Chikawe
2. Ofisi ya Rais - Mahusiano na Uratibu: Stephen Wassira
3.Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma: Hawa Ghasia
4. Ofisi ya Makamu wa Rais - ( Muungano): Samia Suluhu
5. . Ofisi ya Makamu wa Rais - (Mazingira): Dr. Terezya Luoga Hovisa
6. Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge): William Lukuvi
7. Uwekezaji na Uwezeshaji: Dr. Mary Nagu
8. Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI): George Huruma Mkuchika
Naibu: Aggrey Mwanri
Naibu: Kassim Majaliwa
9. Wizara ya Fedha: Mustapha Mkulo
Naibu: Gregory Teu
Naibu: Pereira Ame Silima
10. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi: Shamsi Vuai Nahodha
Naibu: Balozi Khamis Suedi Kagasheki
11. Wizara ya Katiba na Sheria Celina Kombani
12. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard K. Membe Naibu: Mahadhi Juma Mahadhi
13 . Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa: Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi
14. Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi: Dr. Mathayo David Mathayo
Naibu: Benedict Ole Nangoro
15. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia: Prof. Makame Mnyaa Mbarawa
Naibu: Charles Kitwanga
16. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi: Prof. Anna Tibaijuka
Naibu: Goodluck Ole Madeye
17. Wizara ya Maliasili na Utalii: Ezekiel Maige
18. Wizara ya Nishati na Madini: William Mganga Ngeleja 1. Adam Kigoma Malima
19. Wizara ya Ujenzi: Dr. John Pombe Magufuli
Naibu: Dr. Harrison Mwakyembe
20. Wizara ya Uchukuzi: Omari Nundu
Naibu: Athumani Mfutakamba
21. Wizara ya Viwanda na Biashara: Dr. Cyril Chami
Naibu: Lazaro Nyalandu
22. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi: Dr. Shukuru Kawambwa
Naibu: Philipo Mulugo
23. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii: Dr. Haji Hussein Mpanda
Naibu: Dr. Lucy Nkya
24. Wizara ya Kazi na Ajira: Gaudensia Kabaka Makongoro Mahanga
25. Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto: Sophia Simba
Naibu: Umi Ali Mwalimu
26. Wizara ya Habari, Vijana na Michezo: Emmanuel John Nchimbi
Naibu: Dr. Fenella Mukangara
27. Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki: Samuel John Sitta
Naibu: Dr. Abdallah Juma Abdallah
28. Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika: Prof. Jumanne Maghembe
Naibu: Christopher Chiza
29. Wizara ya Maji: Prof. Mark James Mwandosya
Naibu: Eng. Gerson Lwinge
0 comments:
Post a Comment