SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Tuesday, October 5, 2010

Uganda haitoondoa askari wake wa kulinda amani nchini Somalia
Msemaji wa jeshi la Uganda (UPDF) ametangaza leo kwamba nchi hiyo haikusudii kuondoa vikosi vya majeshi yake katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM). Ijumaa iliyopita Umoja wa Mataifa ulitoa ripoti inayolituhumu jeshi la Uganda na nchi kadhaa za Kiafrika kuwa zilitenda jinai za kivita, mauaji na kuwaunga mkono waasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kati ya mwaka 1993 hadi 2003. Katika radiamali yake dhidi ya ripoti hiyo Sammy Kutesa Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Uganda Jumapili alitishia kwamba wanajeshi wa nchi hiyo ambao wako katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu wataondoka nchini humo. Hata hivyo msemaji wa jeshi la Uganda Felix Kulaigye amekanusha habari hiyo na kusema kuwa askari wa Uganda wanaendelea kuwasaidia ndugu zao wa Somalia. Karibu askari 5,000 wa Uganda wako mjini Mogadishu nchini Somalia chini ya mwavuli wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika AMISOM.

0 comments:

Post a Comment