Mbunge wa Uholanzi mwenye chuki na Uislamu afikishwa mahakamani
Geert Wilders Mbunge wa Uholanzi mwenye chuki na Uislamu leo amependishwa kizimbani kujibu mashtaka yanayomkabili ya kuchochea machafuko na chuki dhidi ya Waislamu pamoja na watu wasiokuwa na asili ya Magharibi. Kesi hiyo ilianza leo mjini Amsterdam na kusikilizwa na Jaji Jan Moors na iwapo mbunge huyo mwenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia atapatwa na hatia atafungwa mwaka mmoja jela au kupigwa faini ya yuro 7,600.
Mbunge huyo pia anakabiliwa na kesi ya kutengeneza filamu ya Fitna iliyo dhidi ya Uislamu ambayo imetajwa na mwendesha mashtaka wa Uholanzi kuwa ni kielelezo cha kuchochea chuki na uhasama dhidi ya Waislamu. Katika filamu hiyo ya matusi na kejeli, Wilders anakitusi na kukivunjia heshima kitabu kitakatifu cha Qur'ani.
0 comments:
Post a Comment