SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, October 6, 2010

Schoenman: Chuki dhidi ya Uislamu inatokana na sera za Marekani

Mwandishi mashuhuri wa Marekani aliyeandika kitabu cha "Historia Iliyofichika ya Uzayuni" Ralph Schoenman amesema chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu inayoshuhudiwa sasa kote ulimwenguni inatokana na sera potofu za nchi hiyo. Mwandishi huyo na mueledi wa siasa za ulimwengu amesema, baada ya kufeli kwa Umoja wa Sovieti na kutopata nguvu ya kuendeleza ubeberu, Marekani imetafuta njia mbadala ya kuendeleza sera zake za ubeberu ili kuweza kuvuruga umoja wa walimwengu. Mwandishi huyo mtajika ameongeza kuwa, nia kuu ya Marekani kuendeleza sera hizo ni kutaka kudhibiti rasilimali na mali asili ya mataifa ya ulimwengu wa tatu. Kura ya maoni ya hivi karibuni imeonyesha kuwa, chuki dhidi ya Uislamu haikuwa imeshamiri katika siku za huko nyuma hususan Marekani lakini chuki hiyo imeenea kwa kasi kubwa kwa miaka ya hivi karibuni kwa madai ya kile wanachokiita vita dhidi ya ugaidi. Schoenman ameashiria kuwa, mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001 nchini Marekani, ni jambo lililopangwa kistratejia na Marekani ili kuendeleza matakwa yake ya kuutenganisha ulimwengu.

0 comments:

Post a Comment