Misri yatoa masharti kwa msafara wa misaada kwa ajili ya Wapalestina wa Gaza
Serikali ya Misri imetoa masharti matano kwa waandalizi wa msafara wa misaada kwa ajili ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza ili kuweza kuuruhusu msafara huo kupeleka misaada hiyo katika eneo hilo. Msafara huo unaoongozwa na taasisi ya misaada ya Viva Palestina yenye makao yake nchini Uingereza hivi sasa uko Damascus mji mkuu wa Syria. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri Hossam Zaky amethibitisha kuwa balozi wa nchi hiyo nchini Syria amewataarifu masharti hayo ya serikali ya Cairo viongozi wa msafara huo. Hata hivyo Zaky hakufafanua masharti yenyewe. Eneo la Ukanda liko chini ya mzingiro wa ardhini, angani na baharini uliowekwa na utawala wa Kizayuni wa Israel tokea mwaka 2007. Serikali ya Misri imeshirikiana na utawala wa Kizayuni katika kushadidisha mzingiro huo kutokana na kufunga mpaka wake wa kuingilia eneo la Rafah ambayo ndiyo njia pekee ya kuingilia Gaza bila ya kukabiliwa na vizuizi vya utawala wa Kizayuni.
0 comments:
Post a Comment