Makamu wa Rais wa Sudan amemkosoa Rais Barack Obama wa Marekani kwa matamshi yake ya kichochezi kuwa damu itamwagika Sudan iwapo kura ya maoni ya kusini mwa Sudan haitafanyika Januari mwakani kama ilivyopangwa.Ali Osman Taha amesema Obama hupokea ripoti kutoka kwa watu wasiofahamu yanayojiri Sudan. Akizungmza mjini Doha Qatar, Taha amesema hii si mara ya kwanza Obama kutoa matamshi hayo ya kichochezi na wala haitakuwa mara ya mwisho. Taha aidha amesema Washington inaunga mkono kugawanyika kwa Sudan. Makamu wa Rais wa Sudan amedokeza kuwa makundi ya Marekani yanayofungamana na utawala haramu wa Israel ndio yanayochochea kujitenga eneo la kusini mwa Sudan.
Sunday, October 17, 2010
Makamau wa Rais wa Sudan akosoa matamshi ya kichochezi ya Obama
Posted by
Ally Shaaban Mgido's
at
Sunday, October 17, 2010
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
0 comments:
Post a Comment