SONYA_FLAWLESS_IMG
WE CREATE GREATNESS. | Professional Networker | Global Business Builder | Health And Wellness Coach | YOUR DREAM OUR PLAN.

Wednesday, October 6, 2010

DK GHALIB BILAL AUNGURUMA MKOANI TANGA


Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na mkewe Bi Asha Bilal, wakati wakiwa ndani ya Kivuko cha Pangani walipokuwa wakivuka kutoka Kijiji cha Mwela kuelekea Pangani mjini jana okt 5.
Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Manispaa ya Tanga mjini, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Tangamano jana, uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unatarajiwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu nchini kote. 
Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akitoa mkono wa pole kwa mwakilishi wa familia iliyopatwa na msiba, baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Kigombe Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga leo mchana na kukuta shughuli za msiba huo uliotokea Kijijini hapo jana.
(Picha na Muhidin Sufiani).

0 comments:

Post a Comment