Marouane Chamakh
MSHAMBULIAJI wa klabu ya Arsenal, Marouane Chamakh anawasili leo usiku akiwa na kikosi cha Morocco kinachokuja kuivaa Taifa Stars katika mechi ya pili ya Kundi D la michuano ya Mataifa ya Afrika kwenye Uwanja wa Taifa Jumamosi, huku wachezaji wawili wakiachwa baada ya kuumia.
Walioachwa ni Nabil El Zhar, mshambuliaji wa klabu ya Salonika ya Ugiriki na beki Adil Kerrouchy wa klabu ya Difaa El Jadida ya Morocco ambao waliumia wakichezea klabu hizo mwishoni mwa wiki na hawatakuwemo kwenye kikosi kilichoanza mazoezi juzi jijini Amsterdam, Uholanzi.
Shirikisho la Soka la Morocco (FRMF) lilitangaza juzi kwenye tovuti yake kuwa wachezaji hao hawatakuwemo kwenye safari ya Dar es Salaam inayoanza leo mchana.
Kwa mujibu wa tovuti ya FRMF, hadi juzi Chamakh, ambaye alikuwemo kwenye kikosi cha Arsenal kilichochapwa mabao 2-0 na Chelsea, alikuwa hajaripoti kambini na hivyo kocha Dominique Cuperly kuanza mazoezi na wachezaji 11 pekee.
Walioanza mazoezi ni pamoja na makipa wa Waydad Casablanca, Karim Fegrouch na Nadir Lamyaghri, na Ahmed Mohamadina wa Olympique Club de Khourigba.
Wengine ni, Michael Basser, Mehdi Benatia , Rachid Soulaimani , Morad Ainy , Youssef Hadji,, Ahmed Kantari , Youssef El Arabi , Adil Hermach.
Wachezaji wengine watatu ambao klabu zao zilicheza mechi Jumapili, waliripoti kambini Jumatatu, nao ni Mounir el Hamdaoui (Ajax Amsterdam), Karim el Ahmadi na Houcine Kharja wa klabu ya Genoa ya Italia.
0 comments:
Post a Comment